Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya jamiI,Jinsia,Wazee,na Watoto,Dkt .Zainab Chaula amewasili katika Kijiji Utoro kilichopo katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kujifunza jinsi ambavyo Kijiji hicho kimeweza kuzuia vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kufungua zaidi ya miaka 20 hakuna kifo kilichotokea .

Juhudi hizo zimetokana na aliekuwa Mganga mfawidhi zahanati ya Uturo kuanzia mwaka 1993 mpaka 2017 Bw. Wilson Chotamganga ,ambaye baada ya kufika kijijini hapo alikuta vifo vingi vilivyotokana na uzazi kwa wakina mama na watoto waliozaliwa ,na watoto hao wachanga walikuwa wakizikwa na wakinamama kwa siri pembeni ya nyumba zao ,ndipo alipoamua kuwatafuta wahudumu wa afya ngazi ya Jamii ambao ni wakinamama maarufu kama Makomandoo ambao hutoa huduma za afya ya uzazi katika jamii toka mama anapogundulika na ujauzito hufatiliwa na kushauriwa kwenye kituo cha afya mpaka atakapojifungua.

Dkt Chaula amesema baada ya kutoka kijijini hapo Wizara yake itaandaa mkakati wa kutoa elimu hiyo kwa kuisambaza Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt .Zainab Chaula amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Uturo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, ya kuwa Wizara yake itahakikisha inafanya maboresho katika Zahanati ya Uturo ili waweze kupata huduma zote za afya na sio huduma za Uzazi pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...