Na Ripota ,Kimataifa 

MELI mbili za mafuta zimeharibiwa ambapo meli moja imeshika moto na nyingine ikiwa inaelea hali iliyosababisha wafanyakazi kuondolewa kutoka meli hizo. 

Matukio hayo ya kutia shaka yametokea hivi karibuni na yanahusu meli hizo za mafuta, huku kukiwa na hali ya wasi wasi mkubwa kati ya Marekani na Iran. 

Taarifa iliyopo kwenye Mtandao wa DW umeeleza kuwa Jeshi la majini la Marekani, limechukua hatua za haraka kutoa msaada kwa meli hizo, na wamiliki wa meli hizo hawakutoa ufafanuzi mara moja wa silaha zilizosababisha uharibifu katika meli zao katika ghuba ya Oman nje ya pwani ya Iran. 

Kwa mujibu wa Wamiliki hao wamesema hata hivyo kuwa meli hizo zimelengwa katika mashambulizi hayo huku Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mashambulizi hayo yaliyoripotiwa wakati Waziri Mkuu wa Japan anafanya ziara nchini humo kwa kiasi kikubwa yanatia shaka. 

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alikutana na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, akitafuta kupunguza hali ya wasi wasi kati ya Iran na Marekani. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...