Jumla ya Sh milioni 190 zimetengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa lililopo karibu na bandari ya Kagunga ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 45.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma, Meneja wa Bandari ya Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, anasema hatua ya ujenzi wa lisema soko hilo unatokana na fursa za kibiashara zilizopo mpakani hapo.

"Katika mradi huu tumefanya kwa kushirikiana na Halmashuari ya wilaya hii kufanya mradi wa ujenzi wa soko ni kufungua fursa za kibiashara katika bandari ya kagunga inayounganisha nchi za Tanzania, Burundi na Congo.

“Pamoja na mambo mengine, bandari hii ni ya kimkakati hivyo ni muhimu kuwa na mazingira mazuri kama miundombuni imara ili kuunganisha nchi hizo tatu kibishara,” anasema

Kuhusu biashara alisema bidhaa nyingi zinazoletwa na meli bandarini hapo zinatoka katika nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Anasema kukamilika kwa miradi huu kutawezesha bandari kupata mapato ya kutosha.

Naye Kaimu Mhandisi wa Bandari ya Ziwa TanganyikaTPA, Injinia Nyakato Mwamnana, anataja kuwa soko Hilo linajengwa na mhandisi mzawa litakuwa la kisasa zaidi kukinganisha na masoko mengine katika ukanda wa kagunga

Akizungumzia ujenzi wa soko hilo, Kidawa Bakari ambaye anafanya biashara ya genge, anasema utawasaidia kukuza biashara zao kutokana na mwingiliano wa wafanyabiashara wengine kutoka Burundi.

"Solo hili likiisha tutafanya biashara hasa siku ya soko, kwani kwa sasa tumekuwa tukipata tabu hasa wakati wa mvua kwani hakuna mahali pa kujikinga," anasema
 Sehemu ya soko la Kagunga linavyoonekana ambalo limekamilika kwa asilimia 45
 Mkandarasi anayejenga Soko la Kagunga akitoa Maelezo kwa Mhandisi wa Bandari.
 Meneja Bandari was Ziwa Tanganyika,Ajuaye Msese akizungumza na Waandishi wa habari juu ujenzi wa soko la kisasa katika Bandari ya Kagunga.

 Kaimu mhandisi wa Bandari za Ziwa Tanganyika Nyakato Mwamnana akieleza namna soko litakavyokuwa likikamilika.
 Kaimu Mhandisi wa Bandari za Ziwa Tanganyika Nyakato Mwamnana akiwa katika mazungumzo na mafundi was soko la Kagunga



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...