Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
ONESHO la tano la  Utalii la Kimataifa nchini (SITE) linatarajiwa kukutanisha wadau wa utalii wa Kimataifa wa ndani  ya nchi zaidi ya 400.

Onesho hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mliman city kuanzia Oktoba 18 hadi 20, mwaka huu utakaowakutanisha wadau wa utalii nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Devota Mdachi amesema washiriki wa maonesho hayo ni mawakala wa utalii wa Kimataifa, waandishi wa habari za utalii wa kimataifa na wafanyabiashsra wa utalii kutoka Tanzania na nchi za jirani.

Amesema washiriki hao wanatarajiwa kutoka nchi zaidi ya 57 Ulimwenguni na  baadhi ya nchi mashuhuri zinazotarajiwa kuleta washiriki ni Marekani, Uingereza, Italia, Ujerumani, Urusi, China, Sweden, Afrika Kusini, Seychelles, Mauritius, Rwanda, Malaysia, Kenya, Thailand, India, Korea ya Kusini na Singapore.

Mdachi amesema maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwani mwaka 2014 kampuni za uoneshaji utalii zilikuwa 40 na mwaka 2018 zimekuwa 152.

Pia amesema wauza safari wakubwa wa kimataifa kwa mwaka 2014 walikuwa 24 na mwaka 2018 walikuwa 335.

"Onesho hili la Swahili Expo limeendelea kupanua wigo wa maeneo ya vivutio vya utalii vya kutembelewa na mawakala wa utalii wa kimataifa ili kuwapatia elimu pana ya vivutio vya utalii," amesema Mdachi.

Ameongeza kuwa onesho hilo limeendelea kuwavutia wafadhili wengi zaidi kutokana na fursa zinazotolewa na onesho hili za kutangaza brand za wafadhili hao.

Amesema onesho hilo pia litakuwa na programu zitakazoongeza mvuto kwa kampuni za uoneshaji na wananchi watakaotembelea onesho.

"Imeandaliwa program maalum ya kuwasaili mawakala wa utalii wa Kimataifa kupitia Balozi za Tanzania, nchi za ng'ambo. Kupitia ushirikiano tunaopata kutokana ofisi zetu za Ubalozi wakitekeleza diplomasia ya uchumi hivyo mawakala tutakaopata watakuwa wenye tija kwa biashara ya utalii Tanzania," amesema Mdachi.

Onesho hilo ni mahusus kutoa fursa za kipekee kwa wakala hao kukutana na mawakala wa utalii wakubwa  pia kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogowadogo kuonesha bidhaa zao  utamaduni wa mtanzania kama vile sanaa za mikono, mavazi, vyakula vya kitanzania na ngoma.
Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Devotha Mdachi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho la tano la Utalii la Kimataifa litakalofanyika mwezi Oktoba baadae. Kushoto kwake ni Mratibu wa Onesho hilo la SITE 2019 Joseph Sendwa na  kulia ni Afisa uhusiano wa bodi hiyo Geoffrey Tengeneza,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...