Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Katavi

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema ni marufuku kwa wanachama wa chama chochote cha siasa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kwasababu ni kosa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu huyo wa mkoa amesema aligundua uwepo wa baadhi ya wanasiasa wanaopita nyumba kwa nyumba kufanya kampeni na kuandikisha kadi za wapiga kura jambo ambalo ni kosa.

Pasipo kutaja chama hicho alisema vyama vyote vinapaswa kusubiri hadi Septemba katika uchaguzi wa serikali za mtaa ndipo waanze kampeni zao kwa mujibu wa sheria.

"Tunatambua kwamba kampeni za siasa zina muda wake hivyo ni kosa kwa chama chochote iwe CCM, TLP, ACT-Wazalendo au Chadema kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kabla ya muda wa kampeni na atakayekamatwa anafanya hivyo atashughulikiwa," amesema RC Homera.

Alifafanua kuwa mikutano ya hadhara ya kisiasa ilipigwa marufuku na Msajili wa Vyama vya Siasa na wanaruhusiwa kufanya mikutano ya ndani.

Katika hatua nyingi pia Homera alipiga marufuku wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya wajasiriamali kusumbuliwa katika maeneo yao wqnayoyofanyia biashara.

Akieleza mafanikio katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho katika mkoa wake Mkuu huyo wa Mkoa alisema alipoingia katika nafasi hiyo alikuta zoezi hilo likiwa limefikia asilimia 5 tu lakini hadi kufikia jana lilikua limefikia asilimia 29.

"Niliingia ofisini Mei 23 mwaka huu na nilikuta ugawaji umefikia asilimia tano lakini hadi sasa tumeshafika asilimia 29 na tunaelekea asilimia 30," amesema Homera.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kusikiliza juu ya Miradi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Pombe Magufuli.
Wanahabari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Juma Homera alipokuwa akizungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mkoa wake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...