Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Usalama wa vyombo vya usafirii wa Baharini na Maziwa unahitaji kuwa na Mafunzo ya mara kwa mara kwa ajili ya vyombo hivyo kwa wataalam ikiwa ni pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali katika uokoaji pindi linapotokea kuweza kukabiliana.

Hayo ameyasema  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilmali Watu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji kwa  Zanzibar Rajab Yakub Uweja wakati akifunga Mafunzo ya  Wataalam wa Usalama na Uokoaji katika usafiri wa Baharini ulioshirikisha nchi Tisa uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Uweja amesema kuwa mafunzo ya usalama katika bahari na maziwa yanahitajika kutokana vyombo vya majini ni muhimu katika sekta ya usafirishaji  nchini.

Amesema kuwa Tanzania bado tuko vizuri lakini mafunzo bado ya yanahitajika kwa wataalam wa usalama na uokoaji.

Aidha amesema kuwa Shirika la Usafiri wa Meli Duniani (IMO) kutokana na utaratibu  wake limeonelea kuja kufanya mafunzo Tanzania kwa kutambua ni moja ya nchi inayopokea Meli  nyingi.

 Nae Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli Nchini (TASAC) Emmanuel Ndomba amesema usalama makosa yanayofanyika katika bahari asilimia 80 ni makosa ya kibinadamu hivyo wamiliki wa meli na vyombo vingine vya majini wanahitaji mafunzo.
Amesema kuwa Tanzania iko vizuri katika udhibiti wa usimamizi katika sekta ya usafirishaji wa Baharini na  Maziwa. 
 Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katondo akizungumza na waandishi wa habari namna Wizara hiyo walivyojipanga katika udhibiti wa  sekta ya usafirishaji katika mafunzo ya wataalam wa vyombo vya usafiri Baharini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Nchini (TASAC) Emmanuel Ndomba akizungumza kuhusiana mafunzo wataalam wa vyombo vya usafiri Baharini yaliyoshirikisha nchi Tisa yaliofanyika jijini Dar Salaam.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdullah Ulega akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Watumishi wa Taasisi wa Sekta ya Uvuvi nchini Somalia wanaopata mafunzo katika Wakala ya Vyuo vya Uvuvi nchini (FETA) Mbegani wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilmali Watu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Rajab Yakub Uweja akizungumza wakati akifunga Mafunzo ya Usalama na Uokoaji kwa wataalam wa vyombo vya usafiri Baharini yaliyoshirikisha nchi Tisa yalifanyika Jijini Dar es Salaam.



 Wadau wa Mafunzo ya Usalama na Uokoaji wa vyombo vya usafiri Baharini wakisiliza mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...