Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa wananchi watumie muda uliopo kujiandikisha kupata vitambulisho vya taifa ili waweze kusajili laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole (biometria).

Kaimu Mkuu Kanda ya Mashariki wa TCRA, Jumanne Ikuja amesema ni vyema wananchi wakafahamu kuwa usajili wa simu ni kwa kutumia kitambulisho cha taifa pekee.

Ikuja amesema awali usajili wa simu ulitumia vitambulisho vya aina tano na kusababisha kuwepo kwa usajili holela na hivyo walishindwa  kudhibiti mawasiliano hayo.

Aidha amesema usajili huo utawasaidia kupata taarifa sahihi za watumiaji wa simu na kuondoa changamoto ya watu waliokuwa wanatumia vitambulisho vya ndugu, jamaa na marafiki pamoja na waliokuwa wanatumia laini bila kuzisajili.

"Lengo  kukomesha uhalifu wa mitandao hivyo tumejipanga hadi Desemba 31, mwaka huu  watanzania wote wawe wamesajili laini zao ili kupata huduma bora," amesema Ikuja.

Aliongeza kuwa wanafunzi waliochini ya miaka 18 ambao bado hawajapata vitambulisho vya taifa watatumia vitambulisho vya wazazi wao na kwamba pindi watakapofikia umri sahihi, watatakiwa kuboresha taarifa zao kwa kupitia mfumo huo.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (NIDA), Thomas Nyakabengwe amesema vitambulisho vya taifa ni muhimu kwani ndicho kinatambulisha uraia na kwamba huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinahitaji mtu kuwa na kitambulisho hicho.

Nyakabengwe alisema hivi sasa mtu anayetaka kubadili umiliki au kumiliki ardhi anapaswa kuwa na kitambulisho hicho, kupata leseni ya biashara na kufungua kampuni.

Amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa katika kupata vitambulisho hivyo kwa sababu ya kusajili laini hivyo wamejipanga kuhakikisha wanasogeza huduma kwa wananchi kadri itakavyowezekana ili wananchi wapate

Alisisitiza wanashirikiana na Idara ya Uhamiaji kuwatambua watanzania ili kukamilisha taratibu za kujiandikisha kupata vitambulisho hivyo.

Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandao, Edga Massawe alisema usajili wa kutumia alama za vidole utawasaidia kuwapata watu wanaofanya makosa ya kimtandao na kuwachukulia hatua za kisheria.

Pia alisema usajili huo utawasaidia kuwabaini matapeli wanaotuma taarifa za kupitia mitandao mbalimbali kuomba fedha kwa watu.

Alisema pamoja na kuhamasisha usajili wa laini pia wanatoa elimu kuhusu  sheria ya mtandao ikiwemo makosa yaliyoainishwa pamoja na adhabu zake ili wananchi waweze kuepuka kujiingiza katika makosa hayo.
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi wa habari wakati maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wananchi wakipata huduma za usajili wa laini simu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...