Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi
tanzania (tpsf) godfrey simbeye
amesema kufuatia nchi kukabiliwa na changamoto ya vijana kukosa ajira kwasababu
ya kukosa sifa kiushindani hivi sasa kunaanzishwa mabaraza ya ujuzi ya kisekta
yenye lengo la kuhakikisha suala la ujuzi linakuzwa kiufasaha kuanzia elimu ya
vyuoni pamoja na kuwezeshwa kwa vijana wabunifu nchini.
Simbeye amesema hayo mjini Morogoro wakati
warsha ya kuandaa wajumbe wa mabaraza ya kisekta yenye nia ya kuwafanya kujua
majukumu yao.Amesema kuwa Tpsf ni moja ya watekelezaji wa
mkakati wa kitaifa wa kukuza ujuzi, na Tpsf ndio inayohusika na kipengele cha
kuunda mabaraza ya ujuzi katika sekta sita ambazo ni muhimu kiuchumi ikiwemo
Kilimo biashara, Utalii, Nishati, Ujenzi, Tehama, na Usafirishaji na zote
zitakuwa na mabaraza ya ujuzi.
“mabaraza yatatakiwa kwenda na spidi ya
teknolojia na mabadiliko yaliyobadilika kwenye viwanda vinavyoendelea na
vinavyoanzishwa nchini, mabaraza yanatakiwa kutafanya tafiti kwa lengo la
kuwafikia vijana wenye vumbuzi mbalimbali” alisema Simbeye.
Pia amesema katika mkakati huo wa kukuza ujuzi
Tanzania TPSF lilidhamilia kuunda baraza la ujuzi la taifa, na nchi kama
Tanzania imechukua hatua nyingine tofauti na imekuwa nchi ya pili kwa bara la
Afrika ambayo imekuwa na mfumo huo wa mabaraza.
Juni 22 mwaka huu waziri wa Elimu Profesa
Joyce Ndalichako anatarajiwa kuzindua mabaraza ya kisekta jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi tanzania (tpsf) godfrey simbeye wapili kutoka kulia kwa walioketi pamoja na wadau wakati warsha ya kuandaa wajumbe wa mabaraza ya kisekta yenye nia ya kuwafanya kujua majuku
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...