Na, Editha Edward-Tabora

Waalimu wa Vyuo vya Uuguzi, maabara, Utabibu pamoja na Afya ya jamii wameiomba Wizara ya Afya Maendeleo Ya jamii jinsia wazee na Watoto  kuangalia uwezekano wa kufanya mapitio ya sheria ya mikopo kwa Vyuo vya afya ngazi ya Astashahada na Astashahada  kupata mikopo ili iweze kukidhi  kutoa Elimu dhidi ya wanafunzi wanashindwa kumudu gharama za masomo

Ameyasema Hayo mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya Nkiga Mkoani Tabora Robert Masano  katika mahafali ya Tano yaliyofanyika leo katika chuo hicho

Dkt. Jackson Kaluzi Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya sayansi Nkiga amesema"kama inawezekana Serikali iangalie suala hili katika Jicho la tatu kwa Sababu hawa ni watanzania hapa Tunaona wakati mwingine vijana wanapata shida kulipa ada inabidi wakati mwingine, Mwanzoni tulikuwa na ufadhili kutoka ulaya Lakini kadri siku zinavyoenda inaonekana hatupati ufadhili wa kutosha "Amesema Kaluzi

Hindu  Salumu na Amani Azack ni baadhi ya wahitimu wa Ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Uuguzi na  maabara katika chuo hicho wamesema Tatizo la mikopo linawapelekea baadhi ya wanafunzi kurudi nyumbani kwa kukosa Ada na  na wengine kurudia muhula na kukosa pesa ya mahitaji  madogo madogo

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo amesema amelipokea suala hilo na ataliwakilisha sehemu husika ili kila Mwanafunzi anayesomea fani za utabibu Uuguzi Afya ya jamii waweze kupewa 
 Mkuu wa chuo cha Sayansi Nkinga Robert Masano akieleza ugumu uliopo katika kuendesha kozi hizi za afya bila mikopo.
 Darubini zinazotumika kupima vijidudu visivyoonekana kwa macho ya kawaida.
 Wahitimu wa fani ya utabibu Uuguzi maabara na Afya ya Jamii wa chuo cha Sayansi za Afya Nkiga wakitunukiwa vyeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...