Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga imetoa mapendekezo kadhaa kwa Uongozi wa Klabu ya Yanga ikiwemo kuanzisha wiki ya mwananchi itakayokuwa inafanyika mwezi wa nane kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga Anthony Mavunde wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO inayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mavunde amesema katika ripoti yao wapendekeza kuanzishwa kwa wiki maalum itakayojulikana kama ‘Wiki ya Mwananchi’, ambayo ni maalum kwaajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga kuitumikia jamii.

Amesema wiki hiyo itakuwa ikifanyika mwezi Agosti kila mwaka na siku ya kilele chake kutafanyika tukio kubwa litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam likiambatana na utambulisho wa wachezaji wao wapya.

“Tumepanga tuwe na Wiki ya Mwananchi’, ambapo wanachama wa Yanga watafanya usafi maeneo katika hospitali, masoko na kutoa misaada mbalimbali. Wiki hiyo ikikamilika tutakutana Uwanja wa Taifa”, amesema Mavunde.

Amesema wamemuomba Rais Magufuli na endapo ataridhia tukio hilo litafanyika mwaka huu ambapo miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kutambulisha wachezaji wao wapya wanane ambao wamesajiliwa kutoka nje ya Tanzania kwaajili ya msimu ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...