Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.


Licha ya Nogwa na maneno ya kumchafua kwenye mitandao ya kijamii, Diamond Platnumz anaendelea ‘kutesa’ katika gemu la muziki wa kizazi kipya humu nchini na sehemu nyingine duniani.

Diamond amekuwa akisafiri kwenda kutumbuiza katika nchi za Bara la Ulaya, Falme za Kiarabu na Asia.Nyota ya msanii huyu inaonesha ipo juu mno kwa kuwa kila sehemu anakokwenda, anakubalika.

Hivi karibuni alimshirikisha mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Fally Ipupa katika wimbo wa “Inama”, unaotamba katika baadhi ya vituo vya redio humu nchini na kwenye mitandao ya kijamii.

Kufuatia umri wake wa miaka 30 hivi sasa, yaelekea siku zijazo ataweza kufanya mambo makubwa mno hata ya kuitangaza nchi yetu kwenye safari zake nje ya nchi.Baada ya kuzaliwa October 02, 1989 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipewa majina ya Nasibu Abdul Juma.

Kwa bahati mbaya hakupata malezi ya baba na mama yake kwakuwa akiwa na umri mdogo, wazazi wake walitengana.Baba yake alimuacha bila msaada wowote ikabidi yeye na mama yake mzazi wahamie Tandale Magharibi kwa Nyanya yake mzaa mama, hapo ndipo yakawa makazi yao.

Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa “Binadamu wabaya”.Mnamo mwaka 1995 alianza kupata elimu ya Checheka katika shule ya Chakula bora iliyopo Tandale Uzuri.

Diamond alipomaliza elimu hiyo, akajiunga na elimu ya msingi mwaka 1996 katika shule ya Tandale Magharibi, jijiniDar es Salaam. 

Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano, Diamond alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kukopi baadhi na kukariri nyimbo za wasanii waliokuwa ‘wakihit’ ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho.

Nasseb akawa anaziimba nyimbo hizo sehemu mbalimbali.Mama yake mara nyingi alikuwa akimnunulia kanda za album za Wasanii tofauti waliokuwa ‘wakihit’ kipindi hicho.Alidiriki hata kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanawe aweze kuzishika na kuimba kirahisi.

Mama huyo wakati mwingine alikuwa akimpeleka katika matamasha tofauti tofauti ya kuonesha vipaji, ili Diamond apate nafasi ya kuimba.Baadhi ya ndugu wa familia yao waliona kama mama yake anampotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo.

Maisha yao yalikuwa ni ngumu sana, kwakuwa mama yake Diamond hakuwa hana njia ya kumuingizia kipato, ilibidi atumie kiasi kidogo anachokipata toka kwa kodi ya vyumba viwili alivyopewa na mama yake yaani Nyanya yake Diamond.

Aidha alikuwa akifanya biashara zake ndogondogo kwa mikopo, ili aweze kumsomeshea na kumlea mwanawe Diamond.Hali ilivyozidi ‘kubana’, walilazimika wote kuhamia katika chumba cha Nyanya huyo, wakapangisha vyumba vile viwili alivyopewa mama Diamond.Baada ya kuhitimu shule ya msingi mwaka 2002, Diamond akataka kuanza masomo ya Sekondari mwaka 2003.

Mama yake alimshauri aachane na mambo ya muziki kabisa, azingatie masomo ili apate elimu itayomsaidia hata katika muziki wake.Mama huyo akamwambia haiwezekani kushika vitu viwili kwa pamoja muda huo.

Diamond akaanza masomo ya sekondari huku akiendelea kufanya muziki kisirisiri bila mama yake kumbaini. Ilipofikia mwaka 2004 taratibu akaanza kujifunza kuandika nyimbo zake mwenyewe.

Baada ya kuhitimu elimu yake ya Sekondari mwaka 2006, mwaka uliofuatia wa 2007 Diamond akajikita rasmi katika shughuri za muziki ili kujaribu kutimiza ndoto zake.Hali ya maisha kwa Diamond aliyoyapitia hayakuwa rahisi kama alivyokuwa akitegemea.Ilifikia muda akaanza kutafuta vibarua sehemu tofauti ili aweze kupata riziki na kuepuka hali ya kushinda nyumbani.

Diamond alipitia kazi ya kuuza mitumba, kuuza mafuta katika vituo vya Shell, kupiga picha, kupigisha simu na kazi za viwandani.Alilazimika wakati mwingine kuingia kwenye makundi ya kucheza kamali za mitaani ili aweze kupata pesa ya kuingia studio kurekodi nyimbo zake.

Juhudi zake hizo hazikuweza kuzaa matunda. Diamond akiwa na ari ya kufikia malengo yake, ilimlazimu kuuza pete ya Dhahabu ambayo alipewa na mama yake mzazi.Baada ya tukio hilo, akamdanganya mama yake kuwa pete hiyo ameipoteza!Alifanikiwa kupata ‘fungu’ lililomuwezesha kuingia studio kurekodi wimbo wa kwanza uitwao “Toka mwanzo”.

Ukosefu wa mazoea ya kurekodi, ulisababisha kushindwa kutengeneza wimbo ambao unao ‘hit’ wapenzi wa muziki.Kwa bahati njema kwake wimbo huo watu walishangazwa jinsi Diamond alivyoingia kwa mara ya kwanza studio na kuweza kutengeneza wimbo kama mtu ambaye ni mzoefu.

Baadhi yao wakaamini kuwa akipata nafasi ya kurekodi mara kadhaa, angeweza kufanya vitu vikubwa zaidi.Wimbo ule ulimfanya aweze kukutana na Chizo Mapene ambaye alijitolea kumsimamia, Wakaanza kurekodi album. Wakiwa katikati ya kurekodi album hiyo anayemsaidia kwa bahati mbaya alipata matatizo ya kifedha na hakuweza tena kumsaidia.

Diamond ilimbidi aanze upya kuzunguuka katika studio tofauti kuomba kusiniwa kwenye rekodi label.Lakini kote alikopita hakuweza kufanikiwa, wote walimwambia bado hajafikia kiwango cha kuimba, wakaacha kumsikiliza kabisa.

Kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana hata yule mpenzi wake ambaye alikuwa naye, alimukimbia baada ya kuchoshwa na ndoto hewa za Diamond ambazo alikuwa akiziota kila siku kuwa ipo siku atafanikiwa kimuziki.

Ndoto za Diamond zilikuwa kuwa atakuja kuwa mwanamuziki mkubwa, yeye na mpenzi wake huyo wataishi maisha mazuri.’Kitendo cha mpenzi wake huyo kilimchanganya na kumuumiza sana Diamond hususan kwa kauli aliyomuambia ya "sikiliza Diamond mi kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana maslahi kwangu".

Kutwa ilikuwa ikimpitia kwenye kichwa chake, akajiona kama mwenye mikosi.Mwaka 2009 Diamond alikutana na Bwana Msafiri Peter maarufu kama Papaa Misifa ambae alikubali kumsaidia kimuziki na Kurecord wimbo wa kwanza ulioenda kwa jina la "Nenda kamwambie".

Wimbo huo aliuimbia kwa uchungu mpenzi wake Sarah Sadiki, aliyemuacha akielezea kiasi gani aliumia kwa yeye kumuacha.“Mungu si Athumani” usemi huu ulijionesha baada ya nyota ya Diamamond kuaza kuchomoza taratiibu.

Nenda Kamwambie ulikuwa ikichukua chati siku hadi siku, maisha ya Diamond yakaanza kubadilika hadi kuweza kununua gari aina ya Toyota Celica.Februari 14, 2010 Diamond aliachia album yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo 10 za Kamwambie , Mbagala , Nitarejea , Nalia na mengi , Binadamu , Nakupa , Usisahau , Uko tayari , Wakunesanesa , Toka mwanzo na Jisachi.

Ilipotimu Aprili 04, 2010, aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tunzo tatu za Tanzania Kili Music Awards.Tuzo hizo za Msanii bora Chipukizi, Wimbo bora wa mwaka Kamwambie, na Wimbo bora wa R&. Tunzo hizo zilimfanya achaguliwe kuwa balozi wa Malaria nchini Tanzania. 

Baada ya kuachia wimbo wake wa pili unaoitwa Mbagala, Diamond alichaguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mshereheshaji katika kampeni za kuwania urais. 

Diamond Oktoba 02, 2010 alipata mwaliko wa kwanza kwenda nchi uingereza katika miji ya London, Milton Keynes na Coventry 

Msanii huyo baada ya kuachia wimbo wake wa tatu mwaka 2011, alishinda Tuzo ya Nzumari Award nchini Kenya, akiwa kama Msanii bora wa Kiume toka Tanzania. Diamond Platnumz alifytaua wimbo wake wa nne, akaweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza na pekee kujaza Club Maisha, hadi watu kushindwa kuingia.

Baadhi ya watu walizirai baada kutokupata hewa ya kutosha kutokana na kujaa kwa ukumbi kupita kiasi.Siku ya mwaka mpya Januari 01, 2012 Diamond Platnumz, aliachia album yake ya pili na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuuza zaidi ya kopi 1200,000 za album.

Wakati huohuo aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kufanya show ya Corporate, iliyoitwa “Diamonds are forever" iliyofanyika Mlimani City, kwa kiingilio cha shilingi elfu hamsini za Kitanzania kwa mtu mmoja.

Katika onesho hilo ambalo alilifanya akiwa msanii peke yake, ziliuzwa zaidi ya tiketi 1,500.Mnamo mwezi wa tano mwaka 2012 , Diamond Platnumz aliweka record ya kuwa msanii wa kwanza kufanya show na kujaza zaidi ya watu 10'000 kwa kiingilio cha 20,000 katika kiwanja cha Darlive huku akishuka na Helicopter kwenye Stage. 

Mwaka huohuo Diamond alifanya ziara yake ya Europe ikiwemo Italy, Holland,Sweden , Greece na kumalizia ziara yake ya arabuni. nchini Masqat Oman. Mwishoni mwa mwaka 2012 ulikua mzuri kwa Diamond Platnumz kwani aliweza kuachia nyimbo mbili kwa mpigo za "Nataka kulewa " na "Kesho " zilizoambata na video zake.

Mwezi wa kumi na mbili mwaka 2012 diamond alitajwa kuwa ni msanii wa kwanza anaelipwa Pesa nyingi kwenye Show toka Tanzania Mwanzoni mwa mwaka 2013, Diamond Platnumz alichaguliwa na Cocacola kuwa Brand Ambassador wa Kinywaji Cha Cocacol.

Diamond akafanya na ziara yake ya kuzitembelea nchi za Afrima Mashariki zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kenya n.k.Aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kufanikiwa kupiga show pekeake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000.

Mnamo June 2013 Diamond alishinda tuzo mbili za Tanzania Kili Music Award, akiwa kama Msanii bora wa kiume Bongoflavour na Msanii bora wa kiume kwa wanamziki wote Tanzania.Julai 2013, aliachia singo yake iliyokwenda kwa jina la Number One, ambayo aliifanyia Video katika mji wa Cape Town South, Afrika ya Kusini chini ya kampuni ya Ogopa Videos.

Nasibu Juma ‘Diamond’ akaweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kuzindua video bila kiingilio katika Hotel ya Serena, akiwa amewaalika CEO's , Mameneja na viongozi toka sehemu tofauti tofauti. Katika uzundi huo akamzawadia gari aliyekuwa mwanamuziki mkubwa nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.

Oktoba 10, 2013, Diamond aliifanya Collabo na msanii toka Nigeria Davido katika ngoma ya Number One, ikiwa ni remix.Baadaye alikwenda nchini Nigeria kwaajili ya kusomea Soko la Afrika Magharibi, pamoga na kushoot video ya wimbo huo kupitia Kampuni ya Capital Dreams iliyo chini ya Director Clarence Peter. 

Wimbo huo ulimtambulisha Diamond Platnumz nchini Nigeria na barani Afrika kwa ujumla, ikamuwezesha kupata kra nyingi kwenye tuzo za kimataifa ikiwemo MTV MAMA.Tuzo ambayo alicheza wimbo huo mubashara akiwa na Davido.

Julai 07, 2014 Diamond wakati akisherekea siku ya kuzaliwa ya mama yake, alimzawadia gari pamoja na kuachia video mbili za Mdogomdogo, aliyoifanyia nchini Uingereza na BumBum, aliyomshirikisha Iyanya kutoka Nigeria aliyoifanyia Afrika Kusini.Video hizo kwa pamoja zilimgarimu Diamond dola 78,000 za Kimarekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...