Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amepiga marufuku wale wote wanofanya biashara ya ununuzi wa kahawa kwa wakulima bila kufuata Mfumo rasmi, ambao kawafananisha watu hao wahujumu na Kangomba, mapema Julai 21, 2019 wakati akizungumza na Wenyeviti wa vyama Ushirika, Wakulima na watendaji wa Serikali Wilayani Karagwe.

Mhe. Gaguti Amesema kuwa hakuna mtu yeyote au mfanyabiashara yeyote mwenye mamlaka ya kununua kahawa kwa Mkulima, biashara hii inafanywa kati ya Msimamizi (Serikali) na Mkulima pekee na sivinginevyo hivyo nakutoa wito wale wanaolenga kwenda kwa wakulima kulangula Kahawa kwa bei pungufu na hata wale wanaokwenda kuwazuia wakulima hao wasinunue kahawa watachukuliwa hatua za kisheria.

"Hakuna MTU ataruhusiwa kwenda Kwa Mkulima akanunue kahawa, hicho kitu hakiruhusiwi na kwa atayekutwa au kukamatwa akifanya hivyo ni kufungwa kamba na moja kwa moja ni mahakamani " amesema Mhe. Gaguti.

Aidha ameongeza kuwa zipo taarifa za moja ya kampuni ambayo imeagiza mawakala huko vijijini kwa ajili ya kufanya hujuma ya kahawa kwa kununua kahawa kwa mfumo usio rasmi ambapo ameagiza jeshi la polisi Mkoani Kagera kuhakikisha watu hao wanakamatwa Mara moja kwani tayari wanajulikana.

Haya yanajiri wakati ambapo Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tayari wapo mkoani Kagera kueneza elimu ya Mfumo Jumuishi, mfumo huo wa malipo wenye lengo la kumnufaisha Mkulima ikiwa ni pamoja na Mkulima kulipwa malipo yake kwa njia za Kibenki ambapo pia watafika katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa. 

Awali Kabla ya Mhe. Gaguti kuongea na Wakulima, Watendaji wa Vijiji pamoja na Wenyeviti wa Vyama vya Ushirika, amefanya ziara ya kutembelea viwanda vya kukoboa kahawa Vya Karim Amri na kujionea jinsi Kiwanda hicho kilivyojipanga vyema kwa ajili ya msimu huu mpya wa kahawa, kwa kuongeza mashine mpya zenye uwezo wa kukoboa kahawa nyingi kwa muda mfupi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti akimsaidia kibarua kuchambua kahawa safi na kuhakikisha haibaki na mawe wala uchafu, tayari kuuzwa kiwandani, pembeni ni Mkuu wa Wilaya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimj na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Godfrey Mheluka.
Pichani Wakulima, watendaji, na wenyeviti wa vyama vya Ushirika vya Wilaya za Karagwe na Kyerwa wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Mkoa Kagera (hayupo pichani) wakati alipowatembelea kuwasikiliza katika kufanikisha msimu mpya wa kahawa
Pichani ni Brigedia Jenerali Marco Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoa hotuba yake wakati alipokutana na kuzungumza na Wakulima, Watendaji na Wenyeviti wa Vyama vya Ushirika Wilayani Karagwe.
Pichani ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kukoboa kahawa cha Karim, Bwn. Karim Amri akitoa ufafanuzi juu utaratibu wa kusafisha na kukoboa kahawa kwa Mhe. Gaguti alipofika kiwandani kwake Omgakorongo Karagwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...