Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo ya hospitali mpya inayojengwa wilayani Itilima Mkoani Simiyu. 

Jafo ameonyesha kufahishwa huko akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.“Hamjamaliza kwa asilimia 100 ujenzi wa hospitali yenu lakini nimeridhika sana kwa kazi nzuri ya majengo yenu,” amesema Jafo. 

Jafo amewataka viongozi na watendaji wa wilaya hiyo kukamilisha ujenzi huo ifikapo Julai 30 mwaka huu. Katika Ziara hiyo, Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga kwa kuwapigania wananchi wake katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Aidha,Njalu ameishukuru sana serikali kwa fedha Sh.Bilioni 1.5 zinazofanikisha ujenzi wa hospitali hiyo sambamba na fedha nyingi za miradi mingine ya maendeleo ikiwemo fedha za ujenzi wa jengo la Utawala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...