*Vijana wajitokeza kufanya usafi na wahaidi kuwa mabalozi bora kuhusiana na madhara yatokanayo plastiki

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
VIJANA kutoka Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam wamejitokeza na kufanya usafi katika daraja la Salender ikiwa nk kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita matumizi ya plastiki pamoja na kutekeleza kampeni iliyozalishwa kupitia utafiti uliofanywa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhusiana na madhara ya taka za plastiki katika bahari ya Hindi.

Akizungumza katika zoezi hilo mhadhiri na mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Lydia Gasper amesema kuwa zoezi la usafi ni endelevu na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililoanza mapema mwezi Juni limesaidia sana na kinachotakiwa kwa sasa ni kuzidi kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya plastiki.

Amesema kuwa utafiti kuhusiana na madhara ya plastiki unaendelea na wanaamini suluhu ya tatizo hilo ambalo linaathiri mazingira na viumbe hasa wabaharini itapatikana.

Aidha amesema kuwa usafi huo ulioshirikisha taasisi ya baba watoto unategemewa kuzaa matunda na hiyo ni baada ya watoto hao kuwa mabalozi kwa wenzao katika kutoa elimu kuhusiana na madhara ya kutumia mifuko ya plastiki.

Baadhi ya watoto hao wameeleza kuwa baada ya kupata elimu kutoka kwa wataalamu hao watayatumia vyema maarifa hayo kwa kutoa elimu kwa vijana wengine kuhusiana na madhara yatokanayo na plastiki pamoja na fursa wanazoweza kujipatia kupitia plastiki hizo.

Utafiti huo umehusisha watafiti wanne kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiwemo Dkt. Lydia Gaspare, Dkt. Rose Massalu, DKt. Benjamin Ngatunga na Dkt. Vicensia Shule.
 Mhadhiri na mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Lydia Gasper  akizungumza na wanahabari mara baada ya kufanya usafi katika eneo la daraja la Salender ambapo amesema kuwa wataendelea na utafiti pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
 
 
Baadhi ya vijana wakiendelea na shughuli ya usafi katika eneo la daraja la Salender, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya taka zilizokusanywa katika kampeni hiyo ya Plastiki noma iliyofanyika leo katika daraja la Salender jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...