Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene amesema anamshukuru Rais John Magufuli kwa kumianini tena na kumpa nafasi tena nafasi ya kuwa Waziri kwenye Serikali yake.

Akizungumza baada ya kuapishwa leo Julai 22,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam Waziri Simbachawene amesisitiza kuwa "Kwa heshima kubwa mimi na familia yangu tunakushukuru sana, kwa kuniamini na kunipa nafasi tena.

"Rais wangu nafahamu nini maana ya kula kiapo ,ni kuahidi kuendelea kuviamini viapo vyote na kuvitunza hadi uzeeni kwanu.Leo kiapo ambacho nimeapa ni cha tano kwangu,"amesema Waziri Simbachawene.

Kuhusu nafasi yake baada uteuzi wa Rais na kisha kula kiapo, amesema anafahamu kuwa nchi yetu inayo matatizo makubwa katika mazingira na kuna fedha nyingi ambazo zinaingia kwa ajili ya eneo la mazingira lakini hazitumiki kama inavyotakiwa.

"Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, hivyo najua changamoto zilizopo katika eneo la mazingira na fedha ambazo zinaingia nchini kwa ajili ya mazingira lakini zinatumika kinyume na malengo ya hizo fedha.Hili nitalisimamia na kuhakikisha fedha za mazingira zinatumika kwa ajili ya mazingira yetu na si vinginevyo,"amesema.

Waziri Simbachawene amesema anafahamu kuwa kuna uharibifu mkubwa wa mazingira katika jami yetu." Nikuhakikishe Rais , kwa kumsaidia Makamu wa Rais kwenye ofisi yake, pamoja na wengine nitakaowakuta ofisini nitashirikiana nao na kutoa mawazo yangu ili kuokoa mazingira."

Amefafanua kuwa suala la mazingira linaweza kuzungumzwa kwa aina tofauti, kwani mazingira kimataifa na mazingira kitaifa.Hivyo atajitahidi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Pia amesema anafahamu analo jukumu kwenye eneo la Muungano na katika eneo hilo atajitajidi kadri ya uwezo wake na hasa kwa kuzingatia yeye ni Mwanasheria na Wakili atatumia kila aina ya maarifa yake kuhakikisha muungano unaendelea kuwa imara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...