Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KUMEKUCHA Sherehe za Siku ya Urembo wa asili Tanzania!ndivyo unavyoweza kuelezea sherehe hizo ambazo zinatarajia kufanyika Julai 27 na 28 mwaka huu.

Taarifa ya Mratibu na muandaaji wa sherehe hizo Antu Mandoza ni kwamba zitafanyika eneo la Life Park Mwenge-Dar es salaam na hakutakuwa na kiingilio.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

Mandoza amesema katika siku hiyo pia watawafundisha wanawake kutengeneza vipodozi vya asili na visivyo na kemikali na watatoa kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile watu wenye ulemavu kushiriki katika maonesho hayo bure.

"Mgeni rasmi atakuwa Juliana Shonza na kutakuwa na maonesho ya Wajasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zisizo na madhara kwa ngozi na nywele , urembo na wajasiriamali wengine watashiriki.Pia kutakuwa na upimaji wa kansa ya shingo ya uzazi na ya titi bure , pamoja na burudani ya muziki, fashion shows ya wasichana naturalist na watoto,"amesema.

Tamasha hilo linalofanyika kwa mara ya pili sasa ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Antu Mandoza @missmandoza lengo kubwa ni kusaidia jamii kuepukana na matumizi ya vipodozi hatarishi vinavyosababisha madhara makubwa kiafya kama vile Kansa na pia kuwapa wanawake hasa wasichana ujasiri wa kujiamini na kujipenda walivyo." Naomba kwa wale ambao wanahitaji ufafanua na maelezo mengine ya ziada tuwasiliane kupitia mawasiliano ya namba za simu 0783324787,"amesema Mandoza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...