Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
BODI ya Nyama Tanzania imesema, mwisho wa kutumia magogo ya kukatia nyama ni Septemba 30, mwaka huu, ambapo atakayekaidi atachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu magogo hayo yanamadhara kiafya, ambayo yanatengeneza mazingira ya kuzaliana kwa wadudu  au vimelea vya magonjwa.

Aidha, imesema magogo hayo pia yanasababisha hasara ya upotevu wa nyama, kitaalamu katika kilo 100 inapotea kilo moja, ambapo kwa mwaka muuzaji anapoteza Sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua machine ya kisasa kukatia nyama.

Hayo yamesemwa leo Julai 5, 2019 na Ofisa Usajili kutoka katika bodi hiyo, Geofrey Sosthenes katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam, ambapo aliwataka wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu.

Amesema watakao kaidi agizo hilo watachukuliwa hatua na Msajili wa bodi hiyo, kwa sababu tayari amekwisha ziandikia mamlaka za Serikali za Mitaa tangu  Februari, mwaka huu kwa maana ya wakurugenzi wa idara zote kuhakikisha wanaboresha maeneo yote yanayizalisha nyama ukiwa pamoja na machinjio, makalo na mabucha.

Ofisa huyo, ameongeza kuwa, hawapendi kuyatumia magogo kwa sababu yanamdhara kutokana na kwamba hayasafishiki, ukiwa unakata nyama baada ya mwezi yanakuwa ni mabaki ya muda mrefu na yanatengeneza vimelea vya magongwa ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa walaji.

Aidha, amesema, utumiaji wa magogo pia husababisha hasara kwani mtu akitumia gogo, Kumbuka anatumia na shoka, kinachotokea nyama inagawanyika.

"Kama una bucha inauza kilo 200 kwa siku unaona ni kiasi gani unapoteza, ukipiga hesabu yak kwa mwaka unapoteza sh milioni 3.8 ambayo inatosha kununua mashine ya kisasa ya kukatia nyama, tunawasihi kuacha kuyatumia magogo kwa sababu si salama kwa afya za watumiaji," alisema Sosthens.

Tutahakikisha tunawashauri wamiliki wa mabucha kuhakikisha wanakuwa na mabucha ya viwango ambayo yapo kwenye sheria, viwango hivyo ni pamoja na kuacha kutumia magogo jambo ambalo tumeisha lisisitiza".

Ofisa huyo pia ametoa ombi kwa wadau wote wanaojishughulisha na mnyororo wa thamani wa nyama au anayefanya biashara hiyo au msafirishaji au mfugaji ahakikishe amesajiliwa na kumiliki cheti kutoka katika bodi hiyo.
Ofisa Usajili wa bodi ya nyama nchini,  Sosthenes akifafanua jambo kww wananchi waliotembelea banda la bodi hii katika maonesho ya 43 ya sababa  yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini  Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...