MSANII wa Bongofleva Rajab a.k.a Harmonize amesema ifike wakati wasanii watambue na waheshimu jitihada za wakongwe na waasisi wa Muziki .

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam leo. Harmonize amesema anatambua mchango wa wakongwe wa Muziki wa Bongofleva na kuwataja Q chillah,Ay,Mwana fa,Ferouz na wengine wengi kuwa ndio moja wa funguo zilizowafanya wasanii wengi kutamani kuingia kwenye kiwanda cha Muziki.

"Wachache sana wenye kutambua juhudi za wakongwe hawa ambapo nchi za nje wasanii wa zamani wamekua wakipewa kipaumbele na kuheshimiwa mfano mzuri Msanii 2 face idibia kutoka nchi ya Nigeria anaheshimiwa sana na wasanii ambao ni chipukizi na wanaofanya vizuri kwa sasa lakini hapa kwetu imekua nadra wakongwe kupewa thamani yao,"

Hata hivyo Harmonize ameamua kutangaza rasmi kurudi kwa Mkongwe wa Bongofleva Abubakar katwila a.k.a Qchillah na kutangaza kazi zake mpya tatu ambazo ameshirikiana na kwenye album yake.

"Wakati nilipokua najifunza kuimba nilikua namtazama chillah kama mfano wa kuigwa na nimepita kwenye nyayo zake kutokana na kipaji chake kuanzia utunzi wake na sauti yake ya kipekee ambayo bado ipo vizuri,"

Aidha, mbali na Harmonize kutangaza rasmi kurudi kwa msanii q chillah pia ameamua kumpatia gari aina ya porte kama zawadi kwake itakayomuwezesha kufanya Safari zake za kimuziki.

"Wakati nampigia chillah aje studio tutengeneze nyimbo kwa ajili ya album yake alisema mdogo wangu nikija utanilipia bodaboda binafsi nilijisikia vibaya kutokana na yeye ni Msanii mkubwa sana na hakustahili kuwa kwenye Hali duni kiasi hicho ndio maana nimeamua kumzawadia gari,"

Kwa upande Mkongwe huyo Q chillah amesema anatambua mchango wa Harmonize kwani ni wachache sana wanaojitoa kwa watu na kuwa na moyo wa kuwasaidia wengine.

Hata hivyo amehaidi kufanya kazi na kurudi kwa kasi zaidi na kuwataka mashabiki wasubiri album yake mpya na nyimbo ambazo amemshirikisha harmonize.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...