Ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na baadhi
ya wakuu wa mashirika ya umma (pichani) wamefanya ziara ya kibiashara nchini Brazil yenye
lengo la kutafuta fursa za kibiashara, uwekezaji na masoko kwa
bidhaa zinozalishwa Tanzania.Ziara hii ilianza tarehe 28 Juni ina itakwenda hadi 08
Julai, 2019.
Ziara hiyo ya siku kumi imebuniwa na sekta binafsi kwa mashirikiano
na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania na kuratibiwa kwa
pamoja na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na Ubalozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia, imejumuisha washiriki kumi na
mbili ( 12) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki,
ofisi ya ubalozi wa heshima wa Brazil nchiniTanzania, jumuiya ya wafanya
biashara Tanzania; kampuni ya Zest limited na Kampuni ya Alpha Group
Afrika. Washiriki wengine katika ziara
hiyo ni kampuni ya KC Land Development Plan, Kampuni ya Pivotec Company
Ltd pamoja na Shirika la biashara la Taifa la Zanzibar(ZSTC), Mamlaka ya
Uthibiti wa Matumizi wa Maji na Nishati Zanzibar(ZURA) na LAM Consultant.
Katika Ziara hiyo ujumbe wa Tanzania umeonana na kufanya mazungumzo na Taasisi
mbali mbali za Brazil zikiwemo shirika kuu la uchimbaji mafuta na
gesi la Brazil (Petrobras), kampuni ya shughuli za idhibiti wa viwango na
uendelezaji wa masoko ya mafuta na gesi (IBP), Wakala wa uwekezaji na
Biashara ya Brazil (APEX), Muungano wa Jumuiya ya Wenye viwanda ya
Brazil(NCI) na Taasisi ya Uendelezaji wa Wazalishaji wadogo na Wakati
(SEBRAE). Taasisi nyingine ambazo ujumbe
huu ulikutana na viongozi na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano ni Bodi ya
Utalii ya Brazil(Embratur), Wizara ya Kilimo, Sehemu ya udhibiti wa biashara za
Mazao ya matunda na mifungo, Muungano wa Wenye viwanda wa São Paulo na Taasisi
ya uendelezaji wa Teknolojia na ubunifu (São Paulo Technlogy Incubator) ya
mjini São Paulo.
Hali kadhalika, ujumbe wa Tanzania ulipata
nafasi ya kutembelea Miji mbali mbali ya Brazil ikiwemo Rio de Janeiro ,
Brasilia, na São Paulo pamoja na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi na
Maofisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brasilia na
kukutana na Jumuiya ya Watanzania (Diaspora)
waishio mjini São Paulo.
Katika mazungumzo na shirika la
uchimbaji wa mafuta na gesi la Petrobras na Kampuni ya uendelezaji wa masoko na
Udhibiti wa mafuta na gesi (IBP) ilibainika kwamba pamoja na kampuni ya
Petobras kusitisha shughuli zake za utafutaji wa mafuta nchini Tanzania, nchi
hizi mbili zinaweza kuendeleza kushirikiana katika maeneo mbalimbali yakiwepo
kujenga Uwezo, kuendeleza utafiti, kukuza masoko na shughuli za udhibiti wa
bidhaa na viwango katika sekta ya mafuta na gesi, pamoja na kubadilishana
uzoefu na wataalamu. Ili kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa
pande mbili ( IBP na Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania-ATOGS )
zimekubaliana kuandaa mkataba wa ushirikiano na kusainiwa mara baada ya
kukamilisha taratibu zinazohitajika.
Kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa
kwa bidhaa za Tanzania kama vile korosho, karafuu na mazao ya bahari kupata
soko nchini Brazil. Pia wajumbe wamebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa
Tanzania kununua sukari kutoka Brazil. Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Brasilia umeahidi kufuatilia upatikanaji wa masoko hayo. Brazil ni mzalishaji
mkubwa wa sukari na mazao ya mifugo.
Katika mazungumzo yaliyohusu
ushirikiano wa uwekezaji kati ya nchi mbili yaliyofanyika katika Makao
makuu ya wakala wa uwekezaji wa Brazil (APEX) mjini Brasília ilibainika kuwa
Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza katika taratibu za kuvutia wawekezaji
kutoka nje na kuendeleza wawekezaji wa ndani. Pia pande mbili zilikubaliana
kushirikiana katika kuendeleza fursa za uwekezaji na kubadilishana Taarifa.
Vile vilewajumbe walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuwa na taarifa za kutosha
kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, hivyo wito ulitolewa kwa ofisi za
Ubalozi wa Tanzania Brasilia, Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania, wakala wa
uwekezaji wa Brazil , mamlaka za uwekezaji Tanzania na jumuiya ya wafanya
biashara na sekta binafsi Tanzania kuimarisha ushirikiano wa karibu sana kwa
lengo la kuimarisha uwekezaji na kukuza biasharakwa maslahi ya maendeleo ya
uchumi wa nchini hizi mbili.
Kutokana na ziara hii, ujumbe wa
Tanzania pia ulipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa Taasisi inayohusika na
kuendeleza wazalishaji wadogo wadogo na wa kati (SEBRAE) nchini Brazil.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika makao makuu ya ofisi hiyo yaliyopo mjini
Brasilia. Baada ya mazungumzo hayo pande mbili zimekubaliana kuimarisha
ushirikiano katika maeneo ya kubadilishana wataalam, uzoefu, na kujenga uwezo
hasa kutokana na nchi ya Brasil kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuleta maendeleo
katika kuimarisha uwezo wa wazalishaji wadogo wadogo na wa kati hasa wanawake.
Pia ujumbe wa Tanzania ulitoa mwaliko kwa Viongozi wa taasisi hiyo na baadhi ya
wazalishaji wa Brazil kutembelea Tanzania mwezi wa Oktoba wakati wa Tanzania
Expo.
Kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa Tanzania na Jumuiya ya Muungano
wa viwanda wa Brazil, pande mbili zimekubaliana kwamba nchi hizi mbili
zinashabihiana kimazingira, kijiografia, mila na utamaduni. Hivyo kuna haja
kubwa wa kuimarisha mahusiano, kubadilishana wataalam, habari, na kukuza
technologia ya uzalishaji katika viwanda. Brazil imeonesha nia ya kusaidia
Tanzania katika kujenga uwezo wa wataaman wake kwa kutumia taasisi zake za
mafunzo ya Technologia na kuendelea uzalishaji katika sekta ya viwanda.
Kwahivyo imeonekana kwamba kuna haja ya kuweka saini makubaliano ya ushirikiano
wan chi hivi mbili kati ya Jumuiya ya Muungano wa Viwanda wa Brazil na Jumuiya
ya sekta binafsi pamoja na Jumuiya ya wafanyabiashara, wenye viwanda na
wakulima wa Tanzania. Hatua hiyo itafikiwa baada ya kukamilisha taratibu za
mikataba ya kimataifa
Kwa upande wa utalii imebainika kwamba licha ya kuwa Brazil na Tanzania kuwa zina
mazingira na vivutio vinavyolingana vya utalii, Brazil inapokea zaidi ya mara
tatu ya idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania. Hivyo Tanzania ina mengi ya
kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Brazil. Wito umetolewa kwa pande mbili
kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu, taarifa na utalamu pamoja na kutembelea
na.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...