Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UJUMBE kutoka Jimbo la Zhejiang nchini China, uko nchini kusaka fursa za uwezekezaji, ikiwamo kukutana na wafanyabiashara wakubwa na wadau wa sekta ya Utalii watakaoweza kushirikiana nao katika uwekezaji maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara kati ya wageni hao na wafanyabiashara wa hapa nchini na wadau mbalimbali, Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa ujio huu wa wageni ni moja ya fursa waliyoipata mwaka jana kwenye ziara ya ya utangazaji baada ya kwenda Nchini China na kuingia makubaliano na kampuni ya Touch Roaf

Mdachi amesema, kampuni hiyo iliwaahidi kuleta watalii 10,000 na katika kundi la kwanza la utalii 343 wameshafika nchini na watalii wengine watafika nchini muda wowote kwa kutumia shirika la ndege la Air Tanzania baada ya makubaliano kati ya Touch Road na ATCL.

Amesema, wanaandaa ziara nyingine ya utangazaji nchini China na watatembelea mikoa yote ili kuongeza fursa ya kutangaza sekta ya utalii hususani upande wa malazi.

PMwenyekiti wa ujumbe huo, Ge Huijun, alisema hatua hiyo inatokana na ushirikiano wa China na Tanzania, ambao umezidi kuimarishwa siku za hivi karibuni.

Alisema jimbo la Zhejiang lenye zaidi ya wakazi milioni 57 lina fursa nyingi za biashara na uwekezaji, lakini pia lina wakazi wengi wenye uwezo wa kuwekeza nje ambao nao wanahitaji kujua fursa zilizopo Tanzania.

Amesema, jimbo lake lina watu wengi ambao wana kipato cha kati na wanahitaji kutalii, wameona Tanzania kuna fursa za utalii na wameanzisha kampeni maalumu ya ‘Travel to Tanzania’ yenye uwezo wa kuleta hadi watalii milioni saba kwa mwaka.

Alisema kupitia kampeni hiyo ya kuwataka watu wao wasafiri na kuja Tanzania kutalii, mapokeo yamekuwa mazuri na katika safari za awali zimetimiza zaidi ya asilimia 80 ya matarajio yao.
Picha ya pamoja ya ujumbe kutoka Jimbo Zhejiang na wafanyabishara na wadau wa sekta ya utaliu baada ya kumalizika kwa kongamano. 
Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumzia fursa waliyoipata kwenye sekta ya utalii kutokana na ziara iliyofanywa mwaka jana nchini China na kufanikisha kuingia mkataba na kampuni ya Touch Road ga kuleta watalii 10,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza kwa niaba ya wafanyabishara na kuzungumzia fursa zinazopatikana nchini Tanzania na kuwakaribisha wawekezaji hao kutumia nafasi hiyo kuja nchini kuwekeza. Hayo aliyasema wakati wa Kongamano la wafanyabishara na ujumbe kutoka jimbo la Zhejiang.
Mwenyekiti wa Ujumbe wa Jimbo la Zhejiang Nchini China Ge Huijun akielezea madhumuni ya safari yao nchini Tanzania, hatua hiyo imetokana na ushirikiano kati ya nchi ya China na Tanzania ulioimarika siku za hivi karibuni
Mwenyekiti wa Bodi wa Utalii Nchini (TTB) Jaji Thomas Miayo akizungumza wakati wa Kongamano la wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utalii na ujio wa ujumbe kutoka jimbo la Zhejiang utakaoboresha sekta ya utalii nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...