Na Chalila Kibuda Michuzi TV
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimesema kuwa vijana wachangamkie kusoma masuala ya Takwimu kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika maonesho ya  14 ya  Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Chuo hicho, Neema John amesema kuwa nchi yeyote ili iweze kuendelea inahitaji kuwa na watakwimu watakaochagiza mipango ya serikali katika kuweka Takwimu sahihi.

Amesema kuwa wanafunzi waliohitimu wasome takwimu kutokana na mahitaji yaliyopo.
Aidha amesema Chuo hicho kwa Afrika ni pekee ambapo watu wanatoka nje wanakuja kusoma.

"Tunataka kuwa na watakwimu wengi nchini ambao ndio wataweza kuweka Takwimu sahihi za kila kitu ili serikali iweze kwenda na takwimu hizo kupanga maendeleo" amesema Neema.
Aidha amesema katika maonesho hayo wanafunzi wapite katika banda la Takwimu kuangalia kozi  wanayotoa kuanzia ngazi ya Cheti hadi shahada pili ya uzamivu.

Hata hivyo amesema kuwa changamoto ya ajira kwa watakwimu ni ndogo sana kutokana na kuwepo kwa mahitaji mengi ya watakwimu.
 Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Neema John akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC)  katika maonesho ya 14 ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mhadhiri Msaidizi na Msajili  wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) John Mganga  akitoa maelezo kwa mwanafunzi walipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Richard Jacob akitoa maelezo kwa mwanafunzi wakati alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...