Viongozi wapya wa Jumuiya Kuu ya Wanzania waishio Uingereza na Ireland ya Kaskazini  “ The Association of Tanzanians in the UNITED KINGDOM (ATUK). Kutoka kulia waliokaa ni  Dkt. Imani Kondo ambaye amechaguliwa kuwa Katibu, katikati ni Bi. Martha Mpangile ambaye anafanya kazi ya uanasheria mjini London amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Watanzania.
Kutoka kushoto ni Bi. Zuhura Adam Sapi Mkwawa Mtaalum wa Hisabati kutoka  mjini Leicester amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Waliosimama kutoka kulia ni Bi. Lucy Shigikile mfanyakazi toka Jumuiya ya Madola London anakuwa Mtunza Hazina, anayefuata katikati ni Bw. Frank Leo CEO wa Upendo Events ya mjini Coventry anakuwa Katibu  Msaidizi na mwisho kushoto ni Bw. Nelson Kampa Real Estates Agent toka Birmingham na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Watanzania waishio Birmingham anakuwa Mtunza Hazina Msaidizi.
Uchaguzi wa Viongozi Wakuu hao ulifanyika katika ukumbi wa Ubalozi mjini London tarehe 14 Julai, 2019. Mhe. Balozi Asha- Rose Migiro ndiye mlezi wa Jumuiya Kuu ATUK.
Mwanasheria Bi. Mpangile atafanya mkutano wake wa kwanza Mjini Birmingham katika ukumbi wa Ibis Style Hotel NEC tarehe  28 Julai, 2019 ambako atakutana na viongozi wapya lakini pia atafanya mazungumzo ya makabidhiano toka Kamati Maalum katika  dhima ya kutekeleza dira na mwelekeo wa Jumuiya Kuu.

Imetolewa na Uongozi ATUK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...