Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Mbunge wa Simanjiro, na kada wa chama cha Mapinduzi ccm,James ole Milly amewataka viongozi wasitaafu serikalini na Chama kuacha kuingilia na kukosoa jitihada zinazofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi badala yake waunge mkono jitihada hizo zinazofanywa na rais John Magufuli katika kuliletea maendeleo taifa.

Milly ametoa Kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha, kufuatia kuibuka kwa baadhi ya viongozi wastaafu nchini kuanza kukosoa na kubeza jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli ambaye ameonyesha uzalendo mkubwa katika kulitumikia Taifa na wananchi wake.

Mbunge huyo amewataja baadhi ya wastaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba na Mzee Abdulrahman Kinana ambao hivi karibuni waliibuka na kuandika waraka wakitumia kivuli cha chama cha Mapinduzi, alidai viongozi hao wastaafu hawana mamlaka ya kufanya hivyo.

Alisema wastaafu hao Mzee Makamba na Kinana hawana uhalali wowote wa kukosoa na kuhoji mwelekeo wa CCM na serikali yake."Ukisoma kwa kina taarifa ya viongozi hawa wastaafu wa CCM utagundua kuwa walikuwa na nia ovu ya kuhujumu na kutokuwa na imani na uongozi wa Rais Magufuli" Alisema Milly.

Amesema taarifa hiyo ni Kuendeleza siasa za kudhalilisha na kuponda juhudi za mabadiliko chanya ya kisiasa ,Kijamii,kiuchumi na kiusalama yaliyoanzishwa na mwenyekiti wa CCM ,Rais Magufuli.

Milly alisema pamoja na kutounga Mkono kauli mbalimbali zinazoibuliwa na wanaharakati ,ila aliwataka Makamba na Kinana iwapo wanabaini shutuma zinazoelekezwa kwao si za msingi ,kukimbilia mahakamani na si kutumia kivuli cha CCM .

Aliwataka wananchi kuepuka kauli za kichochezi zinazoenezwa na wastaafu hao kwa kuwa zinalenga kuigawa CCM na serikali yake na kuwataka wananchi wamuunge mkono rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR),mradi wa Umeme wa maji ya mto Rufiji (Stickers Gorge ,Ununuzi wa ndege 8 na ufufuaji wa shirika la Ndege nchini (ATCL).

Aliwataka viongozi wasitaafu kumwacha huru rais Magufuli ili atekeleze ahadi alizozitoa kwa wananchi na kuepuka kumwingiza kwenye misukosuko na migogoro ya kisiasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...