Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kazi uliofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 5 Julai 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kazi uliofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo tarehe 5 Julai 2019. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba na Steven Kihwele ambaye ni mchumi Wizara ya Kilimo.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dar es salaam 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) leo tarehe 5 Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry katika kikao kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam. 

Katika mkutano huo Mhandisi Raouf amemueleza Mhe Hasunga kuwa lengo la ziara yake ni kuangalia uwezekano wa kutumia fursa inayopatikana na kutolewa na Benki ya EXIM inayotoa mikopo nafuu ili kufanya biashara kati ya nchi za Afrika. 

Amesema kuwa akipatiwa mkopo huo ataongeza uwezekano wa kusambaza mbolea na viuatilifu ili kuongeza tija na kasi ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya wakulima. 

Kwa uoande wake Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemueleza Mhandisi Raouf kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutekeleza kwa vitendo hivyo ina wakaribisha  awekezaji katika uwekezaji mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda vya kusindika mazao. 

Alisema kuwa Mhe Magufuli amejipambanua katika kuimarisha uwezekano wa wawekezaji kuwa na uwekezaji uliotukuka ili kuwanufaisha watanzania sambamba na manufaa kwao wenyewe. 

Katika mkutano huo baina ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TOPIC ya Mjini Cairo nchini Misri Mhandisi Raouf Bakry ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mbolea ya Taifa (TFC) Ndg Salum Mkumba. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...