NA Mwandishi Wetu Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewaagiza viongozi wa Wizara yake kuachana na semina katika sekta ya Afya na badala yake wawekeza fedha zao katika vyuo vya Afya ili kupata Wanafunzi wenye ubora.

Dkt. Chaula amesema hayo wakati alipotembelea Chuo cha Uuguzi Milembe kilichopo Jijini Dodoma ili kuongea na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo kwa lengo la kubadilishana mawazo lakini pia kupata maoni kutoka kwao.

Aidha Dkt. Chaula ameongeza kuwa fedha za semina zinawanufaisha watu wachache lakini zikiwekezwa kwa wanafunzi wa Afya wanapata elimu yenye ubora ambayo matokeo yake hutoa huduma bora za tabibu kwa watu wengine. 

Dkt. Chaula amewapa moyo wanafunzi hao kutokata tamaa na badala yake wafanye kazi na kusoma kwa bidii ili hapo baadae waje kuwa viongozi wa Taifa hili kama ilivyo kwa viongozi wa sasa ambao pia wametokea kwenye fani ya Afya.

Dkt. Chaula amewataka wanafunzi hao kukabiliana na changamoto zilizopo na kuwataka kuiga na kufuta yale mazuri na kuachana na mabaya akiongeza kuwa katika maisha lazima kuwe na changamoto.

Dkt. Chaula aliongeza kuwa zamani shule ziliwaandaa wanafunzi kuwa wazalendo kwa kuwafundisha stadi za maisha akitaja mfano wanafunzi kujifunza shughuli za kilimo wakiwa wa shule kwa kuwapingia kazi za kumwagilia bustani.

Aidha Dkt. Chaula aliwataka wanafunzi pamoja na uongozi wa Chuo kuwa wabunifu ili mambo yaweze kwenda akiongeza kuwa kiongozi mzuri ni yule anayekuja na matokeo na kuacha tabia ya kusubiri serika kufanya kila jambo kwani hakuna serikali ila kuna viongozi wenye dhamana wanaowajibika kwa wananchi.

Wakati huo baadhi ya wanafunzi waliotoa maoni yao kwa kiongozi huyo walitaka kujua vigezo vya kujiunga na mafunzo chuoni hapo ambapo mwanafunzi Jacline James alioji kwanini kiwango cha matokeo ya kuingilia chuni hapo kushuka hadi alama D tofauti na awali ambapo mwanafuzi alidailiwa na kiwango cha ufaulu cha angalau C mbili na D moja lakini aliondolewa wasiwasi kwamba Chuo hicho kidaili wanafunzi kwa vigezo vya NACTE.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na Wakurugenzi walio chini ya Wizara yake  akiongea na wanachuo  wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.
Wanachuo wa Chuo cha uuguzi Milembe Dodoma walimsikiliza  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...