BARAKA Jackson kutoka Mkoa wa Manyara ameibuka kuwa Bingwa katika fainali za Mashindano ya Pool siku kuu ya nanenane yajulikanayo kama “Kenice 88 Pool Competitions 2019” yaliyomalizika jana jijini Dar es Salam katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyama kwa kumfunga Festo Yohana kutoka Mkoani Dodoma 7-4 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki saba(700,000/=).

Baraka alipata ushindi huo kutoka katika mkusanyiko wa wachezaji 64 kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania katika mchezo huo wa mfumo wa mchezaji mmoja mmoja (singles) ambao ni mwaka wa tano sasa ukiandaliwa na mdau wa mchezo wa Pooltable katika siku kuu nanenae kila mwaka, Michael Machela na kuratibiwa na Chama cha Pool cha Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni.

Festo Yohana(Dodoma) kwa kufungwa fainali hiyo alishika nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki tatu(300,000/=).

Akizungumza na wachezaji,mashabiki pamoja na wadau wote waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni, Mathayo Mathemba aliishukuru Kampuni ya kutengeneza meza za Pool ya Kenice kwa kuendelea kudhamini mchezo huo na kuwaomba waendelee kuwashika mkono kwani kupitia wao wanaamini ipo siku watapata mdhamini wakuweza kuurudisha mchezo huo kwenye hadhi yake kama ulivyokua.

Mathemba alisema, Wachezaji tuigeni nidhamu ya mchezo aliyoionyesha Bingwa wa mwaka huu toka tumeanza mashindano ambaye kwa sasa yuko Kenya anaishi vizuri kwa kucheza mchezo huu nchini Kenya pamoja na kwamba familia yake iko Mkoani Manyara.

Nai Bingwa wa mashindano ya Kenice 88 Poool 2019, Baraka Jackson alimshukuru muandaaji, Michael Machela, wadhamini Kampuni ya kutengeneza meza ya Kenice, waratibu Chama cha Pool Mkoa wa Kinondoni(KIPA) pamoja na wachezaji wote waliojitokeza mwaka huu na akasema kilichomfanya mpaka apate ubingwa ni hasira ya kukosa ubingwa katika kipindi cha miaka mine yote iliyopita hivyo aliamua kwenda kuweka kambi Kenya kwa maandalizi rasmi ya ushindi alioupata alisema Baraka.

Baaraka alisema, katika mchezo wa Pool hakuna uchawi bali ni mazoezi sana na nidhamu ya mchezo ndio yatakayokufanya ufanye vizuri siku sote katika mchezo huu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...