Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa 39 Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaoanza Agosti 17-18 mwaka huu upatikanaji wa maji ndani ya Mkoa Wa Dar es Salaam na viunga vyake umezidi kuimarika. 

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamejizatiti katika kutoa huduma ya maji safi kwenye maeneo yote Jijini wakati wote wa mkutano huo utakaowahusisha viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika. 

Hayo yamewekwa bayana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuelekea kwenye mkutano huo mkuu ambapo kwa Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yamehitimishwa jana kwa kufungwa Rais wa Zanzibar Dkt Alli Mohamed Shein. 

Luhemeja amesema, maboresho yaliyofanyika ni urekebishwaji wa miundo mbinu yote ili iweze kufanya usambazaji wa maji kwa kiwango cha juu, kuhakikisha mitambo yote ya uzalishaji maji inafanya kazi ili kuhakikisha maji yanapatikana muda wote bila kukosekana. 

DAWASA wamezidi kuimarika katika utoaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya muda mrefu iliyo chakavu, kujenga miradi mipya ya maji na kuwafikia wananchi wote waliokuwa hawapo kwenye mtandao wa maji hususani maeneo ya pembezoni. 

Kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam unapata maji kutoa Mtambo wa Ruvu juu, Mtambo wa Ruvu chini, Mtoni na Visima. 

Katika mkutano huu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa SADC.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...