Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Klabu ya Simba Imefanikiwa kuanza vyema msimu wake mpya baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
 Katika mchezo huo uliokusanya umati wa mashabiki waliosheheni Uwanja wa Taifa, shujaa wa Simba SC alikuwa ni mshambuliaji wake wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere aliyefunga mabao yote matatu ya timu yake.

Katika mchezo huo ulioanza majira ya saa 12 jioni ilichukua dakika tatu ya mchezo kwa Mshambuliaji wa Kimataifa Meddie Kagere kuifungia timu yake goli la kuongoza akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.
 Dakika ya 23, Jimmy Dlingai anaisawazishia Power Dynamos kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Larry Bwalya kumtungua kipa Beno Kakolanya.

Mpaka mapumziko timu hizo zimeenda zikiwa zimefungana 1-1. Kipindi cha pili  ilifanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yote yakifungwa na Kagere
 Kwenye  dakika ya 58 kwa kichwa akimalizia pasi ya winga mpya, Deo Kanda aliyesajiliwa kutoka TP Mazembe na dakika ya 73 akiandika bao la tatu.

Baada ya mchezo huo, Simba watasafiri kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, UD do Songo Jumamosi, kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo wa marudiano kati ya Agosti 23 na 25.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Beno Kakolanya, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Shomary Kapombe/Said Ndemla dk85, Tairon Santos Da Silva/Kennedy Juma dk87, Pascal Wawa, Muzamil Yassin, Deo Kanda/Rashid Juma dk75, Sharaf Eldin Shaibob/Gerson Fraga ‘Viera’ dk49, Meddie Kagere, Clatous Chama na Francis Kahata/Miraj Athumani ‘Madenge’ dk61.
 Power Dynamos; Lawrence Mulenga, Larry Bwalya, Raphael Makubuli, Jimmy Dlingai, John Soico/Clifford Saudi dk75, White Mwamambaba, Benson Sakala, Kondwani Chiboni/Faustin Bakodica dk51, Christian Ntouba/Judo Bolondio dk59, Fredrick Mulamba/Jackob Phiri dk54 na Kassimu Titus/Lameck Kafwaya dk 67.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...