Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna
kila sababu ya kuendelea kutolewa elimu ya usalama barabarani na
matumizi sahihi ya barabara zetu ili kupunguza ajali zinazosababisha
ulemavu na vifo kwa watu wasio na hatia nchini.
Pia
amesema kwa sasa Wizara hiyo ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya
sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea ukali sheria hizo
ili kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto na hasa bodaboda ambao
wengi wao wamekuwa wakivunja sheria mara kwa mara na kusababisha ajali
ambazo zinaweza kuepukika.
Mhandisi
Masauni ameyasema hayo wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi na shule
za msingi ambazo zimeshinda michoro yenye ujumbe wa usalama barabarani
visiwani humo kwa mwaka 2019, ambapo Shule ya Msingi Mkunazini imepata
kitita cha Sh.milioni nne kutoka kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania
baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.
Mafunzo
hayo ya elimu ya usalama barabarani yamefadhiliwa na Kampuni ya Mafuta
ya Puma Tanzania ndio mara ya kwanza kutolewa visiwani humo.
"Kuna
umuhimu mkubwa wa jamii yetu ya Watanzania kwa upande wa Bara na
Visiwani kuendelea kupatiwa elimu inayohusu uslama barabarani pamoja na
matumizi sahihi ya barabara zetu.
"Hivyo
nitumie nafasi hii kuipongeza Kampuni ya Puma Tanzania kwa uamuzi wake
wa kutoa elimu hii ambapo kwa hapa Zanzibar shule tano za msingi
zimepata elimu hiyo na tunaamini itasaidia kupunguza ajali ambazo
zinaweza kuepukika,"amesema Mhandisi Masauni.
Ameongeza
kuwa kutolewa kwa elimu ya usalama barabarani kwa wafunzi kutasaidia
kuokoa maisha yao na kuwapusha na ajali kwani watakuwa na uelewa mzuri
wa kutumia barabara zetu.
Ametumia
nafasi hiyo kuzungumzia mikakati ya Serikali katika kuendelea
kukabiliana na ajali za barabarani nchini na moja ya mkakati ni pamoja
na kusimamia sheria zilizopo na kuongeza wanaendelea na mchakato wa
kupitia upya sheria za usalama barabarani ili ziwe kali zaidi.
"Ajali
za barabarani zimeendelea kupungua siku hadi siku, lakini bado
kunachangamoto ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto na hasa
waendesha bodaboda wanavunja sana sheria za barabarani.
"Tumeamua
atakeyakamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani awekwe mahabusu
na kisha apelekwe mahakamani ili sheria ichukua nafasi yake.Wanavunja
sheria kwa kuamini sheria sio kali sana, sasa tumeamua na tutawadhibiti
ipasavyo kwa watakaoendelea kutoheshimu sheria zilizopo,"amesema.
Awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Ltd Dominic Dhanan amesema
kuwa elimu ya usalama barabarani imetolewa kwa shule tano za msingi za
Zanzibar.
"Tumekutana
hapa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi
walioshinda shindano la michoro ya Usalama barabarani kwa mwaka 2019
kisiwani Zanzibar.
"Tukio
hili la utoaji zawadi linahitismisha prgramu iliofanywa na kampuni ya
Puma kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la AMEND kupitia
New vision Consortium trainers ya Zanzibar wa kutoa elimu ya usalama
barabarani,"amesema.
Amefafanua
programu hiyo ilihusisha mafunzo kuhusu usalama barabarani katika shule
za Msingi Mwembeshauri, Kisiwandui, Shule ya Msingi Jang’ombe, Shule ya
Msingi Nyerere na Shule ya Msingi Mkunazini.
"Wanafunzi
wasiopungua 6500 wamapeta elimu hiyo ambayo imekwenda sambamba na
uchoraji wa michoro inayohamasisha matumizi sahihi ya barabarani na
kufuata sheria zilizopo,"amesema.
Ameongeza
programu hiyo ya usalama barabarani ni mwendelezo wa kampeni ambayo
ilizinduliwa rasmi mwaka 2013 ambapo zaidi ya shule 80 zimefikiwa na
jumla ya wanafunzi 106,500 wamepata mafunzo katika mikoa ya Dar es
Salaam, Geita, Ruvuma, Dodoma na sasa visiwani Zanzibar.
Ametumia
nafasi hiyo kueleza Kampuni ya Puma ya Tanzania imeamua kufika visiwani
Zanzibar kwa sababu ya ukuaji wa shughuli za utalii na za kiajamii
ambazo zimesababisha ongezeko la watu na magari ambayo yanahatarisha
usalama wa watoto wanapokwenda shule na kurudi nyumbani.
"Lengo
kubwa la mpango huu ni kuwafanya watoto hawa kuwa na uelewa wa matumizi
ya barabara wakiwa bado wadogo.Kwa kufanya hivyo tunawaongezea uelewa
kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa waTanzania wengi
zaidi,"amesema Dhanah.
Kwa
upande wake Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mkunazini ambaye ameibuka
ushindi wa kwanza kwa mwaka 2019 kwa kuchora mchoro bora wenye ujumbe wa
usalama barabarani Raya Zuberi Hemed ambaye amejinyakulia Sh.500,000
ameishuku kampuni ya Puma kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi atakuwa balozi
wa kueleza matumizi sahihi ya alama za barabarani.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa
Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma, Dominic Dhanah (watatu
kushoto) na Mrajisi wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed
Khalid Abdullah (watatu kulia) wakikabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi
Milioni Nne kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mkunazini baada ya mwanafunzi
Raya Zubeir Hemed(kulia), kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Shindano la
Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani kwenye hafla
iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa
Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimpa
zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini, Saidat Jumbe zawadi
baada ya kujibu swali lililohusiana na Kanuni za Uvukaji wa Barabara ili
kuepuka ajali.Hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma ya
kukabidhi zawadi kwa washindi wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya
Elimu ya Usalama Barabarani iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa
Baraza la Usalama Barabarani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni, akimkabidhi
kikombe mshindi wa kwanza wa Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu
ya Usalama Barabarani mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mkunazini Rayah
Zubeir Hemed.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya
Puma,Dominic Dhanah.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma,Dominic Dhanah, akimkabidhi
zawadi Mshindi wa Pili Salum Ali Khatib baada ya kushika nafasi hiyo
katika Shindano la Uchoraji wa Michoro ya Elimu ya Usalama Barabarani
lililodhaminiwa na kampuni hiyo.Hafla hiyo imefanyika Visiwani
Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mrajisi
wa Jumuiya sisizo za Kiserikali Zanzibar, Ahmed Khalid Abdullah
akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwandui,Salma Ali
Seif baada ya kujibu swali lililohusiana na usalama barabarani, wakati
wa Hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...