Na Emmanuel Masaka,Michuzi TV
WILAYA Kigamboni jijini Dar es Salaam imesema inatarajiwa kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wa Gezaulole iliyopo Kata ya Somangila katika mwaka huu mpya wa bajeti ili kuondokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi wa kata hiyo kutokana na malipo hayo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Charles Lawiso wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo ya Kigamboni kililofanyika leo Agosti 22,2019 ambapo pamoja na mambo mengine lilipongezwa kwa ufanisi mzuri katika kuiletea maendeleo manispaa hiyo.

Wakati wa kikao cha baraza hlilo la madiwani, Fransis Masanja ambaye ni Diwani wa Kata ya Somangila alitumia kikao hicho kuuliza swali la kutaka kufahamu ni lini wananchi hao watalipwa fidia zao baada ya maeneo yao kuchukuliwa kwa ajili ya mradi wa upimaji viwanja miaka miwili iliyopita.

Hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema Manispaa hiyo imekuwa ikilipa fidia hizo kwa wananchi hao kila mwaka kwa kadri ambavyo fedha zimekuwa zikipatikana.

Ambapo amesema kwa mwaka huu malipo hayo yataanza kutolewa wakati wowote ikiwa ni baada ya mwaka mpya wa fedha kuanza.

"Taratibu kwa ajili ya ulipaji wa fidia hizo zinaendelea, kilichochelewesha hatua hiyo ni kuanza kwa mpango husika unaohusiana na mwaka huu wa fedha, ila kila kitu kipo sawa matarajio yetu wananachi hao watalipwa fedha zaoo,"amesema Masanja.

Katika hatua nyingine manispaa hiyo imesema changamoto ya kukosekana kwa huduma ya choo katika Shule ya Sekondari Kisota inatarajiwa kutatuliwa karibuni.

Akifafanua kwenye hilo la ujenzi wa choo, Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kigamboni Paskazia Tibalinda amesema wanatarajia kukamilika rasmi kwa moja ya chemba ya choo hicho yanatarajiwa kujulikana Jumatano.

Ameongeza uamuzi uliochukuliwa na Manispaa hiyo ni kumtaka Mkandarasi husika kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo hadi Jumatano vinginevyo manispaa itafanya kwa fedha zake kisha kumakata fedha mkandarasi huyo.

Katika kikao cha baraza hilo, kimeelezwa kutokana na changamoto hiyo wanafunzi wa sekondari hiyo wanalazimika kwenda kujisaidia choo cha shule iliyojirani.

Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni, Maabad Hojja akizungumza na waandhi wa habari mara baada ya kumaliza kwa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilicho fanyika leo kililofanyika leo Agosti 22,2019 jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv).
Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kigamboni,Paskazia Tibalinda akifaafnua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo kilicho fanyika leo kililofanyika leo Agosti 22,2019.

Mkutano ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...