Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwapokea majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kuanguka.
Magari yaliyobeba majeruhi kutoka mkoani Morogoro yakiingia MNH.
Wataalam wa MNH wakimweka mgonjwa kwenye kitanda kwa ajili ya kumpatia matibabu.
Madaktari na wataalam wengine MNH wakimuhudumia mgonjwa wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
Mmoja wa majeruhi akipelekwa katika chumba cha matibabu
006: Wataalam wa MNH wakiendelea kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto.
Maandalizi ya kupokea wagonjwa yakiendelea Muhimbli.
Wataalam wakipokea wagonjwa ili kupatiwa matibabu zaidi. 


Na John Stephen


Majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kuanguka, usiku huu wamepokelewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi na wataalam wa MNH.

Majeruhi wameanza kupokelewa MNH saa 4:30 usiku wakitokea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako watu kadhaa wamejeruhiwa kwenye ajali na kupelekwa MNH kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Gari la kwanza la wagonjwa lililobeba majeruhi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro lilingia Muhimbili saa 4:30 usiku na kufuatiwa na magari manne yaliyoingia saa 5:10 usiku na ilipofika saa 6:30 tayari wagonjwa 25 walikuwa wamepokelewa na kuanza kupatiwa matibabu na wataalam mbalimbali wa MNH.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa MNH, Bw. Aminiel Aligaesha amesema kuwa baada ya kutokea kwa ajali mkoani Morogoro, MNH ilituma wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuongeza nguvu wakiwamo madaktari bingwa wa magonjwa ya dharura, Dkt. Juma Mfinanga.

Bw. Aligaesha amesema Muhimbili imetuma wataalam wa upasuaji kwa wagonjwa walioungua moto, madaktari bingwa wa upasuaji na madaktari bingwa wa usingizi ili kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kutoa huduma kwa majeruhi pamoja na kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wanaopaswa kuhamishiwa MNH.

“Kwa upande wetu, tumeandaa madaktari 28, wauguzi 64 na wahudumu wa kawaida 10. Pia, tumeandaa vitanda 89 na kati ya hivyo vitanda 21 ni vya wagonjwa watakaohitaji uangalizi maalumu,” amesema Bw. Aligaesha.

Mbali na maandalizi haya, vile vile MNH imeandaa dawa za kutosha vikiwamo vitendanishi vyote vinavyohitajika kuhudumia majeruhi ambao wameanza kupatiwa huduma mbalimbali za matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...