Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAVETERANI wa timu za Yanga na Simba wanatarajia kunogesha Tamasha la Mtaa kwa Mtaa litakalofanyika Mkoani Lindi kwa kucheza Mchezo wa Kirafiki.

Tamasha hilo limeandaliwa na Mashujaa Fm ya Mkoani humo litawashirikisha wachezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba waliocheza miaka ya nyuma.

Akizungumzia Tamasha hilo, Mkurugenzi wa Masoko Maxmilian Luhanga amesema tamasha la mtaa kwa mtaa limehusisha timu za mpira wa miguu zaidi ya 100 kutoka vitongoji vyote vya mkoa wa Lindi.

Amesema, timu zimeshafikia hatua ya fainali na siku ya Jumapili Agosti 18 mwaka huu itapigwa mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

“Timu takribani 100 zimeshiriki, na fainali itakuwa ni tarehe 18 mwezi huu ila kabla ya mchezo huo kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya wachezaji wa zamani wa Yanga na Simba utakaopigwa Agosti 17, “ amesema.

Luhanga ameeleza kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubww, kikubwa amewaomba mashabiki wa mpira wa miguu mkoani Lindi kuja kuwashuhudia wachezaji wa zamani wa timu za Yanga na Simba pamoja na mechi ya Fainali itakayopogwa kesho yake.

Kwa upande wa wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘machinga’ amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanamfunga mtani wao Simba kwenye mchezo huo wakitaka kulipa kisasi kwa kufungwa kwenye mechi ya bonanza la Serebuka hivi karibuni.

Naye Thomas Kipese mchezaji wa zamani wa Simba amesema kuwa watani zao Yanga wanawafahamu vizuri tu na hata miaka ambayo wakiwa wanacheza waliwafunga ila katika mchezo huo wanataka kuendeleza historia yao ya kushinda kama kwenye mchezo uliopita.

Mshindi wa kwanza wa mechi hiyo ya fainali atapata gari aina ya Noah.
Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Fm Maxmilian Luhanga akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kirafiki wa maveterani wa Yanga na Simba pamoja na fainali ya tamasha la Mtaa kwa mtaa linalofikia tamati Agosti 18 Mkoani Lindi.
Wachezaji wa Zamani wa Yanga na Simba wakiwa kwenye picha ya pamoja pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Fm Maxmilian Luhanga wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar
Mchezaji wa Simba wa zamani Thomas Kipese akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga utakaofanyika Agosti 17 Mkoani Lindi
Mchezaji wa Yanga wa zamani Mohamed Hussein ‘Machinga’ akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya watani wao wajadi Simba utakaofanyika Agosti 17 Mkoani Lindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...