Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMATI ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), imesema jumuiya hiyo itaendelea na harakati za kuishinikiza Jumuiya ya Kimataifa ili kuiondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2019 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Palamagamba Kabudi amesema kamati hiyo itaendeleza harakati za kuishinikiza jumuiya hiyo ya Kimataifa kuondolea vikwazo Zimbabwe.

Profesa Kabudi ambaye amekabidhiwa nafasi hiyo ya Uenyekiti leo ameeleza umuhimu wa Zimbabwe kuwa huru katika shughuli za kichumi kwa kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.

“Zimbabwe imewekwewa vikwazo vya kuichumi kwa muda mrefu , na sasa hakuna sababu ya vikwazo hivyo kuendelea.Hivyo umefika wakati wa kuondolewa vikwazo vya kiuchumi,”amesema Profesa Kabudi.

Prof. Kabudi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefafanua zaidi Zimbabwe imefanya uchaguzi mkuu wake na imempata Rais, hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kuondolewa vikwazo vya kiuchumi ili waendelee kuijenga nchi yao.

Kuhusu mambo mengine yatakayofanywa na kamati hiyo Mwenyekiti huyo wa kamati ya baraza la mawaziri amesisitiza namna Tanzania itakavyotumia nafasi hiyo kuzihamasisha nchi za SADC kutumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya mawasiliano kwa nchi wanachama.

Wakati huo huo Profesa Kabudi amezungumzia umuhimu wa kuhakikisha nchi za jumuiya hiyo zinatafuta ufumbuzi wa changamoto ya uhaba wa ajira kwani asilimia 60 ya vijana katika nchi hizo wanakabiliwa na changamoto hiyo.

“Tutashirikiana kuweka nguvu kwenye eneo la viwanda ambalo tunaamini mbali ya kuleta maendeleo kwa nchi za SADC, pia tutapunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwani wananchi wetu,”amesema Profesa Kabudi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),Profesa Palamagamba Kabudi.Picha na Michuzi JR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...