Naibu Waziri wa Mifugo Kilimo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo na wananchi wa Longido Kata ya Ngarnenairu Mkoani Arusha.

Naibu waziri wa Mifugo,Kilimo na Uvuvi akisikiliza kero za wafugaji katika mnada wa Ngarenaiboru uliopo wilaya ya mkoani Arusha
Naibu waziri wa Mifugo,Kilimo na Uvuvi akisisitiza jambo alipokutana na wananchi wa kata ya Ngarenaiboru katika mnada wa Ngarnaiboru leo.



Na.Vero Ignatus,Arusha

Naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mhe,Abdallah Ulega ametoa agizo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha kuwa kila penye mnada wa mifugo lazima pawe na mizani kama hawatafanya hovyo watanyang'anywa fursa ya kuuza ng'ombe.

Akizungumza katika kata ya Engaranaiboru katika ziara yake ya kikazi wilayani Longido mkoani Arusha,Ulega amesema kuwa uuzwaji wa mifugo Nchini kwa kutumia madalali una lengo la kumnyonya mfugaji na sio kunufaika.

Amesema kuwa 95% ya wakazi wa Longido ni wafugaji hivyo lengo kuu ni kusimamia haki ya mfugi kwani halmashauri nyingi zinachukua mapato katika minada lakini hawafanyi shughuli yenyewe ya kuhuidumia.

Amesema mfugaji anakosa sauti kutokana na mtu wa tatu ambaye ni dalali,ambaye ananufaika wakati aliyefuga ni mtu mwingine.Aidha Ulega amesema Sheria ya kila bidhaa kupimwa ipo wazi na mwogozo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi upo wazi hivyo Mizani ni lazima ili haki ya mfugaji Ipatikane.

Hata hivyo amesema kuwa ikiwa kila mnada utaanza kutumia Mizani itapelekea wafugaji kubadili uelekeo kwa kufuga mifugo michache,yenye tija badala ya kufuga mifugo mingi.

Naye mbunge msaafu Jimbo la Longido Lekule Ole Laizer ameiomba serikali iwapelekee dawa kwaajili ya majosho kwani yapo ila hayatumiki ,pia ameomba wapatiwe kibali cha kuuza mifugo Kenya kama ilivyo kwa biashara nyingine

Lekule amesema changamoto kubwa waliyonayo ni mifugo yao kushambuliwa na magonjwa kama vile Ormolo,kichaa cha mbwa,brusele( Mfugo kutupa mimba),ndigana baridi na moto, Nemonia, ugonjwa wa mapele na mkojo wa damu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...