Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa akiwa katika mzungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi. Mazungumzo hayo yamefanyika kando na mkutano wa TICAD7 Yokohoma,Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi(hayupo pichani) Yokohama, Japan.
Mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi kuhusu wakimbizi waliopo Tanzania yakiendelea. Yokohama, Japan.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao kuhusu wakimbizi waliopo Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika Yokohama, Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandimara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mhe. Kassim M. Majaliwa. Yokohama, Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiteta jambo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw Filippo Grandi mara baada ya kumalizika mazungumzo ya Waziri Mkuu mhe. Kassim M. Majaliwa. Yokohama, Japan.


SERIKALI ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) katika kutatua changamoto zinazotokana na uwepo wa wakimbizi nchini pamoja na kutafuta suluhu ya kudumu kwenye nchi zao ili wakimbizi hao waweze kurejea makwao kuendelea na shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Ijumaa, Agosti 30, 2019) katika mazungumzo yake na Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bw. Filippo Grandikwenye Kituo cha Maonyesho cha Yokohama nchini Japan baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7).

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa UNHCR kuisaidia mikoa inayokaliwa na wakambizi kutokana na kuharibiwa kwa mazingira. “Hata hivyo Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na UNHCR kuimarisha ulinzi wa maeneo ya wakimbizi ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na utulivu.”

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Bw. Filippo Grandi amesema amefurahishwa na utayari wa Serikali ya Tanzania katika kupokea wakimbizi na usikivu wa Rais Dkt. John Magufuli katika kushughulikia changamoto za wakimbizi. 

Waziri Mkuu yupo nchini Japan akimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano wa Kilele wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 7) ambao umehitimishwa leo.

Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...