Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Klabu Bingwa Timu ya Simba imeondolewa katika mashindano baaada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya UD songo ya Msumbini.

Mabingwa wa ligi ya soka ya TPL, wameondolewa kwa goli la ugenini baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Msumbiji kutoka suluhuya kutokufungana.

Katika daika ya 14, Luiz Misquissone aliifungia UD Songo goli la kuongoza baada ya kupiga faulo nje kidogo ya eneo la hatari.

Simba walishindwa kutumia nafasi walizozipata kwenye kipindi cha kwanza baada ya safu ya ulinzi ya UD Songo kuwa makini na kuondosha hatari hiyo.

Mpaka timu zinaenda mapumziko, UD Songo walikuwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Simba.

Kipindi cha pili kilianza kila upande wakitafuta nafasi, Simba wakizidisha mashambulizi langoni mwa wapinzani wao ila umakini unakuwa mkubwa kutoka kwa walinzi wa timu hiyo na kuondoa mipira ya hatari langoni mwal.

Penalti ya dakika za lala salama iliopigwa na Erasto Nyoni haikutosha kuisaidia timu hiyo ya Msimbazi Reds huku Songo ikifuzu katika raundi ya pili kutokana na goli la ugenini.

Kocha wa Simba Simba Patrick Aussems amesema kuwa, wameumia baada ya kushindwa kwenda hatua inayofuata ila kwa sasa watajipanga zaidi katika Ligi Kuu ili wafanye vizuri na kuchukua ubingwa tena.

Kwenye mchezo huo Simba walifanya mabadiliko katika dakika ya 41 kwa kumtoa kiungo wa kati wa Kenya Francis kahata na kumuingiza Hassan Dilunga, Shiboub na kuingia Miraji Athumani na Beki Gadiel Michael na kuingia Mohamed Hussein.

Kwa sasa Tanzania itaendelea kuwakilishwa na Yanga waliofanikiwa kutinga hatua inayofuata ya michuanoya Klabu Bingwa baada ya kuifunga Township Rollers kwenye mchezo wa mkondo wa Pili nchini Botswana goli 1-0 ambapo latika mchezo wa mkondo wa kwanza walitoka na sare ya 1-1 Uliochezwa dimba la Uwanja wa Taifa.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho, Azam wamefanikiwa kutinga raundi ya pili baada ya kuitoa Fesal Kenam kwa jumla ya goli 3-2.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...