Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAPANDA baiskeli kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo kwa lengo la kuitangaza jumuiya hiyo pamoja na na utengamano.

Wakizungumza leo Agosti 21,2019 jijini Dar es Salaa mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, wapanda baiskeli hao wamesema lengo lao ni kuhakikisha wanapeleka ujumbe kwa wananachi kuifahamu vema jumuiya hiyo.

Kiongozi wa wapanda baiskeli hao John Balongo amemueleza Waziri Kabudi wamekuwa wakifanya hivyo kwa nia njema na wanaamini hiyo itasaidia kuifanya jamii kuwa na uelewa kuhusu jumuiya hiyo.

Pamoja na kufafanua kwa kina kuhusu ziara hiyo kwa nchi hizo, amesema changamoto kubwa waliyonayo ni fedha kwani hawana wafadhili zaidi ya kutumia fedha zao mfuko au kupata msaada kutoka kwa nchi za Afrika Mashariki.

"Ombi letu kubwa ni kupata ufadhili kwani itatusaidia kufanikisha safari yetu hii.Tunaenda kwenye nchi zetu kwa kutumia fedha za mfuko, hivyo tutashukuru kama tutapata msaada wenu,"amesema Balongo.

Kwa upande wake Waziri Kabudi amewapongeza kwa uamuzi wao wa kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo na kuwataka waendelee na moyo huo.

"Ni jambo jema kuitangaza Afrika Mashariki na utengamano.Hata hivyo hili la kupata msaada wa kifedha Serikali inao utaratibu wake , hivyo nitalifikisha ili utaratibu wa Serikali utumike,"amesema Waziri Kabudi.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akimkabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mratibu wa Waendesha Baiskeli wa Tanzania, Morris Manyori, kwa ajili ya wapanda Baiskeli wa 'East African Bicycle Tour' wanaofanya Tour ya kuzunguka katika Nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Muungano na umuhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo walianzia Uganda, Kenya na sasa wamefika Tanzania.  Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. 
WAPANDA baiskeli kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kufanya ziara ya kutembelea nchi hizo kwa kutumia usafiri huo kwa lengo la kuitangaza jumuiya hiyo pamoja na na utengamano.Pichani waendesha baiskeli hao wakiwasili leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam,ambapo Waziri Kabudi aliwakabidhi bendera.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akimkabidhi Bendera ya Tanzania, Mratibu wa Waendesha Baiskeli wa Tanzania, Enock Bernad , kwa ajili ya wapanda Baiskeli wa 'East African Bicycle Tour' wanaofanya ziara ya kuzunguka katika Nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Muungano na umuhimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo walianzia Uganda, Kenya na sasa wamefika Tanzania. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Viunga vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Idara ya Miundombinu  na Huduma  za Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Eliabi Chodota  akizungumza jambo mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki, Prof. Palamagamba Kabudi,leo jijini Dar
Kiongozi wa wapanda baiskeli hao John Balongo akisoma hotuba yao kwa Waziri Kabudi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...