Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa (kushoto) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul na Ofisa kutoka wizara ya Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa. Kushoto ni ofisa kutoka Wizara ya Afya na na kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul.




Na John Stephen

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa na kujadiliana kuhusu kushirikiana katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika mazungumzo hayo pande mbili zimependekeza kushirikiana pamoja katika uwekezaji wa viwanda vya dawa na chanjo, kubadilishana wataalam wa afya ili kuwajengea uzoefu wataalam wetu katika nyanja mbalimbali za sekta nchini.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu kwa pamoja wamekubaliana kwa pamoja kuendeleza mapambano ya Homa ya Ini aina C (Hepatitis C) ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora na kwa wakati kuhusu homa ya Ini aina C.

Baada ya majadiliano hayo Waziri Ummy Mwalimu aliagiza kuandaliwa kwa hati ya ushirikiano (MOU) kwa ajili ya kuratibu na kutekeleza maeneo mbalimbali ya kipaumbele katika sekyta ya afya nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...