Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa iliyopo katika tarafa ya kibengu alipotembelea kujua changamoto za shule hiyo. 
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akisalimiana na wananfunzi wa shule ya msingi Kisusa
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisusa


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MBUNGE wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametumia zaidi ya shilingi 81,667,221 katika ukarabati na ujenzi wa shule za msingi za tarafa ya kibengu iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara katika tarafa hiyo Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Mapanda amesaidia ukarabati na ujenzi wa Madarasa mawili shule ya msingi Mtwivila Saruji 90 na fedha kiasi cha shilingi jumla ya shilingi laki sita na nusu,shule ya msingi ukami saruji 70 na rangi kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo.

“Saruji mifuko 220 imetumika katika ukarabati na ujenzi wa madarasa katika shule za msingi ya Chogo,Ihimbo na Uhafiwa pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya uingizaji wa umeme katika shule ya msingi Uhafiwa zote hizo ni juhudi zangu” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa katika kata ya Kibengu amechangia jumla ya mifuko 210 ya saruji,bati 280,madawati 10 na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kuboresha elimu katika shule ya msingi Kibengu,Igomtwa,Kipanga,Igeleke,Usokami na Ilogombe.

Aidha Mgimwa alisema kuwa kata ya Ihalimba inajumla ya shule za msingi nne ambazo ni Vikula,Ugesa,Nundwe na Ihalimba ambapo ametoa saruji mifuko 50 bati 310 na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 44,932,221 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya msingi Ihalimba pamoja na utengenezaji wa madawati 60 kwa ajili ya shule zote za kata hiyo.

“Hizi zote ni juhudi zangu binafsi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi tub ado hapo sijaelezea kuhusu shule za sekondari lakini unakuta watu wamekaa tu vijiweni wanasema mbunge hajafanya kitu sasa hivi wewe mwandishi umejine kwa macho na umewasikia wananchi wenyewe kwenye mikutano ya hadhara” alisema Mgimwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...