Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwasha umeme katika moja ya nyumba za Mkazi wa Kijiji cha Muheza katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha ikiwa ni kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakili Julias Bundala Kalolo( kulia) kabla ya kuwasha umeme na kuzindua Mradi wa Kusambaza umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji ( Peri-Urban) katika Halmashauri ya Kibaha vijijini mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akikata utepe kuashiria kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa miji( Peri-Urban) katika Kijiji cha Mwanabwito wilayani Kibaha vijijini.Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Wajumbe bodi ya Wakurugenzi ya REA ,Viongozi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ikiwemo REA na Tanesco.
Wasanii wa nyimbo za asili kutoka kabila asili ya Mkoa wa Pwani,wakiigiza kumtambikia Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( kulia aliyekaa) wakati wa sherehe za kuzindua Mradi wa Usambazaji wa Umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa miji( Peri-Urban) wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
Gari lililobeba nguzo mali ya Mkandarasi Sengerema zikiwa tayari zimewasili katika kijiji cha Mwanabwito, katika Halmashauri ya Kibaha vijijini kwa ajili ya mradi wa Peri-Urban.

……………………………………………………………..

Na Zuena Msuya, Pwani

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema zaidi ya wateja 6000 mkoani Pwani wataunganishiwa umeme wa mradi wa kusambaza umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji.

Mgalu alisema hayo, Augosti 05,2019, wakati akiwasha na kuzindua umeme katika kijiji cha Muheza katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha na katika kijiji cha Mwanambwito katika Halmashauri ya Kibaha vijijini.

Alisema kuwa maeneo yote ya Wilaya ya Kibaha ikiwemo mitaa, vijiji pamoja na vitongoji vyate vitafikiwa na Mradi wa Peri-Urban.

Alifafanua kuwa mradi huo utangarimu zaidi ya shilingi bilioni 14 katika Mkoa wa Pwani pekee na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuanza kwa utekelezaji wake.

Aliweka wazi kuwa mradi huo utaleta tija kubwa kwa taifa kwa kuwa utakuwa ukifanya kazi ya kuwaungashia umeme wananchi ambao hawakupitiwa na Mradi wa kusambaza umeme vijijini( REA) au hawakuweza kupata huduma hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

“Mradi huu utafanya kazi kubwa sana kwa wananchi na utaleta manufaa makubwa sana kwa sababu wale wote walioshindwa kuunganishwa na umeme wa REA kwa namna moja au nyingine, au wale ambao hawakupitiwa kabisa, sasa mradi huu unamaliza kila kitu, utawaunganisha wote,jiandaeni kuupokea”,alisisitiza Mgalu.

Aliwaeleza wananchi wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kuwa wataunganishwa na mradi huo kwa bei ya shilingi 27,000/= tu,ambayo inajumuisha gharama za nguzo, nyaya pamoja na LUKU, hivyo wananchi wasikubali kuchangia zaidi ya kiasi hicho cha fedha.

Sambasamba na hilo aliwaeleza kuwa mwananchi atalipia gharama ya kutandaza nyaya katika nyumba yake,kwa makubaliano na wakandarasi au mafundi waliothinishwa na shirika la Umeme nchini (TANESCO), kufanya shughuli hizo.

Mradi huu kwa Mkoa wa Pwani unatekelezwa na mkandarasi mzawa wa kampuni ya Sengerema na tayari ameanza kutekeleza mradi huo kwa kuwaungaishia wananchi huduma ya umeme huku akiendelea na ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...