Na said Mwishehe,Michuzi TV

MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Jaji mstaafu Thomas Mihayo amewabana wasanii na watu maarufu ambao wenyewe hawako tayari kuutangaza vivutio vya utalii hadi wapewe fedha au posho na Serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu, wasanii, watu marufu na wadau wa sekta ya utalii nchini Jaji Mihayo amesema kuna wasanii bila kulipwa fedha hawataki kutangaza utalii.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuangalia namna ya kufanikisha kampeni ya kuutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia kundi hilo la wasanii na watu maarufu.

Amesema mbele ya wasanii hao kuwa anakerwa sana na watu ambao wanaoomba kuwezeshwa kwenda kwenye vivutio vya utalii."Hivi ukifanya tamasha ukaweka kiingilio cha Sh.5000 hupati fedha za kwenda huko? 

"Hili ni suala la uzalendo lakini nashindwa kuelewa kwanini hamjiamini kuwa mnaweza kufanya kitu kikubwa kupitia majina yenu".

Amesema haoni sababu ya msanii kupewa fedha ndipo ashiriki kufanya jambo la uzalendo kwa nchi yake na kuongeza wasanii wanao uwezo mkubwa wa kutumia sanaa yao kupata fedha ikiwemo fedha ya kumuwezesha kwenda katika vivutio vya utalii kufanya kazi zake au kupumzika.

“Watanzania wenyewe tuwe na hamu ya kuifahamu nchi yetu na kuwa mabalozi wa kuwaambia watu wengine kuhusu vitu vizuri vinavyopatikana hapa,”amesema Jaji Mihayo.Kwa upande wake Msanii wa Bongo Fleva Nurdin Bilal a.k.a Shetta ametumia nafasi hiyo kueleza mazingira magumu yaliyopo nchini pindi msanii anapohitaji kuredi kazi yake katika hifadhi za taifa na maeneo ya utalii.

Amesema kuwa ndio maana wengi wanakwenda kuredi nje ya nchi ambako kuna mazingira mazuri na mpangilio ambao unaeleweka wa msanii kufanya kazi."Kuna nyimbo ambayo nilienda kurekodi Dubai siku za karibuni.Nilieleza yale ambayo nahitaji yawepo katika nyimbo nikaambiwa gharama yake ni dola 200, hivyo nikalipa na kazi ikaenda haraka tu maana hakuna kucheleweshana kwa kuwa kila kitu kinaeleweka.

"Huku kwetu mazingira bado hajakaa vizuri, hivyo ni vema Wizara ikaweka utaratibu ili msanii anapohitaji kufanya kazi yake iwe rahisi,"amesema Shetta.Awali akizungumza kwa niaba ya wasanii, Msanii Mwijaku ametoa rai kwa wasanii wenzake kujitolea kuwa mabalozi wa kutangaza kazi zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo bila kutegemea kulipwa.

Wakati Msanii mkongwe katika muziki wa kizazi kipya nchini Seleman Msindi a.k.a Afande Sele amezungumzia umuhimu wa wasanii kuimba nyimbo ambazo zitahamasisha utunzaji mazingira na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda a.k.a Fid Q akisalimiana na Peter Msechu baada ya kukutana katika kikao kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu kujadili kampeni ya kutangaza Utalii ndani na nje ya nchi kupitia wasanii na watu maarufu
Ofisa Masoko kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Mariam Kobero akifuatilia majadiliano kati ya wasanii ,watu maarufu na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo(wa pili kulia waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu pamoja na wasanii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...