Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Sehemu ya wabanguaji wa korosho wakifatilia mkutano wa waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) wakati wakati akizungumza kwenye mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wasindikaji Wakubwa na wadogo wa korosho uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma tarehe 9 Septemba 2019.


Na Issa Sabuni, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amewaambia Wasindikaji wadogo na Wakubwa wa korosho kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe Dtk John Pombe Magufuli ni kuongeza kiwango kikubwa cha usindikaji kuliko ilivyokuwa mwaka jana na kwamba Serikali haitanunua tena korosho bali itaweka mazingira mazuri kwa Wafanyabiashara kununua zao hilo kutoka kwa Wakulima bila ya kuwalalia.

Mhe Hasunga ameyasema hayo katika mkutano wake maaalum alioutisha tarehe 9 Septemba 2019 katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma lengo likiwa ni kuzungumza na Wasindikaji hao ili kujiandaa na msimu mpya wa ununuzi wa korosho ambapo taarifa rasmi ya Wizara itatolewa hivi karibuni.

Waziri Hasunga amesema licha ya Serikali kuendelea na azma yake ya kuongeza thamani ya zao la korosho kwa kuwasisitiza Wabanguaji kuongeza ukubwa wa mazao ya korosho kwa kusindika zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.

“Tumeona kabla ya kutangaza taarifa rasmi ya Wizara yenye kuzindua rasmi msimu mpya wa ununuzi wa korosho, ni vyema tukutane nanyi Wadau ili kujadiliana namna nzuri ya kuboresha biashara ya korosho kwa lengo la manufaa ya Wakulima wetu” Amekaririwa Waziri Hasunga

Katika hotuba yake; Waziri Hasunga ameelekeza kuwa Wabanguaji hao wanapaswa kutoa Taarifa kwa Wizara kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020 katika maeneo kadhaa ikiwemo teknolojia wanazotumia katika ubanguaji na usindikaji wa korosho, uwezo wa mashine zao kusindika kwa mwaka, idadi ya Wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda, uwezo wa viwanda kubangua na kusindika korosho kwa mwezi na kwa mwaka vilevile mapendekezo ya bei ya kununulia kabla ya msimu kuanza.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa Wasindikaji pia wanapaswa kuwa wa wazi katika kuishauri Serikali namna nzuri ya kuboresha zoezi zima la ununuzi mpya wa korosho na kueleza changamoto wanazokutana nazo.

Awali katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Bwana Francis Alfred amesema uzalishaji wa korosho kwa msimu huu unataraji kufikia tani laki 3 na nusu (350,000) na kuongeza kuwa tija itaongezeka ikiwa sehemu kubwa ya uzalishaji itabanguliwa na kusindikwa hapa hapa nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...