Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amewataka wasanii na watu maarufu nchini Tanzania kutumia akaunti za mitandao yao ya kijamii kuutangaza utalii wetu.

Pia amewahakikishia kuwa Wizara hiyo ipo tayari kushirikiana nao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kupata kibali pindi wanapohitaji kurekodi kazi zao za sanaa au kwenda kutembelea hifadhi za mbuga za wanyama na utalii.

Kanyasu amesema kuna kila sababu ya kundi hilo kutumika kutangaza utalii wa Tanzania na kuongeza amekutana na wasanii na watu maarufu ili wajadili kwa pamoja nini kifanyike kuendelea kuvitangaza utangaza vivutio vya utalii hasa kupitia kundi la wasanii na watu maarufu.

"Naamini kila msanii au mtu maarufu akitumia vema akaunti yake ya mtandao wa kijamii kutangaza utalii wetu na vivutio vilivyopo tutalifikia kundi kubwa sana.Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kushirikiana nanyi katika hili kwa wale ambao watajitolea kuwa mabalozi wa utalii,"amesema Kanyasu.

Akifafanua zaidi kuhusu mikakati ya Wizara kuutangaza utalii wa Tanzania, Kanyasu amesisitiza umuhimu wa wadau wa sekta ya utalii zikiwemo hifadhi za taifa kushirikiana na wasanii na watu maarufu ili kuongeza idadi ya watalii kuja nchini kwetu.

Ametumia nafasi hiyo kuwashauri wasanii kutumia fursa hiyo kuzitangaza kazi zao za sanaa na wakati huo huo kuutangaza utalii.

“Katika nchi yetu kuna vivutio vingi na vizuri ambavyo wasanii wetu wanakila sababu ya kuvitumia katika kazi zao. Kuna wasani wa hapa hapa kwetu hawapendi kuvitangaza vivutio vyetu, wapo tayari kutangaza vivutio vya nchi nyingine.Hivyo tumewaita ili tujadiliane kwa pamoja,"amesema Kanyasu.

Amesisitiza umuhimu wa watu maarufu na wasanii kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za taifa, na wakiwa huko matukio ambayo wanayafanya wawe wanaweka picha za matukio yao katika akaunti zao za mitandao ya kijamii ili wengine waone.

“Ikitokea msanii au mtu maarufu ukienda mbuga ya wanyama ukipiga picha na kutweet ukaeleza ulipo, watu wengine watatamani kufika hapo,"amesema.

Ameongeza Wizara hiyo inaweza isiwe na fedha kwa ajili ya kuwapa wasanii na watu maarufu lakini uwezo wa kutoa kibali na kulipia usiku mmoja lakini kwa maana anayekwenda atangaze utalii wetu, wako tayari.

“Uzalendo ni pamoja na kuwa tayari kufanya chochote kwa ajili ya nchi yako na mimi niko tayari kumsaidia msanii yeyote anayetaka kwenda kufanya kazi huko aje nitamuunganisha muhimu ni kufuata taratibu,”amesema Kanyasu.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akizungunza na wasanii na watu maarufu nchini jijini Dar es Salaam kuhusu namna Bora ya kufanikisha kampeni ya kutangaza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi nchi .
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akisalimiana na moja ya wadau wa Utalii nchini wakati wa kikao kati kati yake na wasanii na watu maarufu kilichokuwa na lengo la kujadili kampeni ya kutangaza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia kundi hilo
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo(kulia) akizungunza jambo wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu na wasanii pamoja na watu maarufu.Kushoto ni Muandaaji wa Shindano la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi
 Ofisa Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Mariam Kobero akizungumza kuhusu Wakala huo unavyotunza misitu na kuhifadhi Misitu wakati wa kikao hicho
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu(katikati aliyeva shanti nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii na watu maarufu baada kumalizika kikao hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...