Benki ya NMB imeendelea kuwa mkombozi kwenye Jamii maeneo mbalimbali hapa Nchini kutokana na kutoa misaada sehemu zenye changamoto kubwa.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani hapa alipozungumza wakati wa kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Benki ya Nmb jana kwa ajili ya Kituo cha afya cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 826 Mpwapwa .

Shekimweri alisema benki ya NMB imeendelea kuwa mkombozi katika Jamii kutokana na kutoa misaada kwenye maneo yenye changamoto kubwa ya mahitaji.

“Mfano ni hivi vifaa tiba mlivyokabidhi leo ,tunajua wote jinsi eneo la kutolea huduma za afya lilivyo na changamoto ,watu ni wengi katika Jamii wanaofika hapa kwa jili ya matibabu,ni kweli benki mnaigusa jamaii moja kwa moja”alisema.

Hata hivyo aliwashukuru NMB kwa kuendelea kutoa misaada katika Wilaya hiyo kwa sababu kwa mwaka huu hiyo ni mara ya tatu kwa kupata msaada wa mabati kwa baadhi ya shule za Msingi pamoja na madawati .

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Nchini Kanali Festus Mang’wela aliwashukuru benki ya Nmb kwa msaada waliotoa kwa ajili ya kituo hicho cha afya cha 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma .

Kanali Mang’wela alisema kituo hicho kinahudumia watu wengi wakiwemo familia za askari,Askari wenyewe na Jamii inayokizunguka Kikosi hicho . Alibainisha kuwa vifaa hivyo walivyopokea vitawasaidia kutokana na kikosi hicho kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha sita wanaofika kwa ajili ya kozi maalumu ya kijeshi ya miezi mitatu tangu mwaka jana.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi alisema wamekabidhi msada huo wa vifaa tiba wenye thamni yash milioni tano. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda vitano vya kawaida ,mashuka 25,magodoro tano na vitanda vya kujifungulia akinamama viwili vyote vikiwa na thamani hiyo.

Mlozi alisema benki hiyo inasaidia jamii katika sekta kuu nne ambazo ni elimu kwa kuchangia madawati na mabati ya kuezekea ,afya kwa kutoa vifaa tiba ,majanga na kutoa elimu kwa wananchi namna ya utunzaji wa fedha .

Hata hivyo alisema mpaka sasa benki hiyo imeshatoa misaada wenye thamni ya kiasi cha zaidi ya sh milioni 110 kwa jamii Mkoa wa Dodoma.
 Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (kulia) akikabidhi msaada wa kitanda, mashuka na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha afya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma. Jana NMB ilikabidhi msadaa wa sh milioni tano wa vifaa hivyo ,wengine ni Mkuu wa Wilaya Mpwapwa Jabiri Shekimweri (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Kikosi Hicho Luten Kanal Mohamed Karuma na mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Festus Mng'wela waliobaki ni staafu wa benki ya NMB.


  Mkuu wa Wilaya Mpwapwa, Jabiri Shekimweri (wa kwanza kushoto)  akipokea msaada wa mashuka pamoja na vifaa tiba kutoka kwa  Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (wapili kulia) akiwa Meneja Mwandamizi Mahusino ya Kibenki na Seriaklia NMB ,Josephine Kulwa(kulia) wakimkabidhi ,msaada huo uliotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha 826 Mpwapwa Mkoani Dodoma, NMB jana  ilikabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya sh milioni tano,katikakati ni  mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali Festus Mng'wela .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...