Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 09 amemkabidhi Mlinda Mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja kitita cha Shilingi Milioni 10 taslimu ikiwa ni sehemu ya Motisha na zawadi ya Kazi nzuri aliyoifanya jana wakati wa Mchezo baina ya Tanzania na Burundi.

RC Makonda amemkabidhi Kaseja fedha hizo mbele ya Kocha wa Taifa Stars, Katibu Mkuu TFF na baadhi ya wachezaji waliomsindikiza ambapo amekipongeza kikosi kizima cha Timu ya Taifa Stars kwa Kututoa kimasomaso kutinga hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2022.

Kwa upande wake Mlinda mlango wa Timu ya Taifa Juma Kaseja amemshukuru RC Makonda kwa kutimiza ahadi aliyoitoa ndani ya Masaa machache ambapo ameeleza kuwa kiasi hicho cha fedha kitamsaidia katika mambo mbalimbali ya kusongesha gurudumu la Maisha.

Itakumbukwa Jana Tanzania iliibuka na ushindi wa Penati 3 - 0 dhidi ya Timu ya Burundi ambapo Mlinda mlango Juma Kaseja alifanikiwa kupangua mkwaju wa Penati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...