Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

 Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu 
MADAKTARI na wauguzi wa Taasisi ya MOI wamemfanyia upasuaji mkubwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi kwa saa tatu na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Taasisi ya MOI imeuarifu umma wa Watanzania kwamba jana Septemba 9,2019 , saa tano usiku  walimpokea Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi baada ya huduma katika ya hospitali ya KCMC.

Taarifa iliyotolewa leo Septemba 10,2019 na Patrick Mvungi wa Kitengo cha Uhusiano  MOI  amesema kuwa baada ya kupokelewa ,wataalam wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.

"Jopo la madaktari bingwa pamoja na wauguzi wa taasisi ya MOI walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa saa tatu kuanzia saa saba usiku hadi saa 10 alfajiri .Upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa .Baada ya upasuaji hali ya Mhashamu Askofu Ruwaichi inaendelea vyema na bado yuko kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU),"amesema Mvungi.

Hata hivyo taasisi hiyo ya MOI imesema inawatoa hofu watanzania wote hususani waumini wa Kanisa Katoliki kwamba hali ya Mhashamu Askofu Rwaichi inaendelea vizuri na kikubwa ni kuendelea kumuombea ili apone mapema na kurejea kwenye majukumu yake ya utumishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...