Ndege iliyowabeba Faru kutoka nchini Afrka Kusini ikishusha baadhi ya mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA, Faru hao wametolewa na Mfuko wa Grumet (GF) kwenda Serikali ya Tanzania
PIX 3: Baadhi ya maboksi yaliyobeba Faru walitolewa na Mfuko wa Grumet.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu akisaini nyaraka muhimu za makabidhiano ya Faru na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Grumet (GF), Stephen Cunliffe mara baada ya kupokelewa kwa Faru kutoka nchini Arusha. 

Na Mwandishi Wetu, KIA
SERIKALI ya Tanzania imepokea Faru Tisa kutoka Mfuko wa Grumet (GF) nchini Afrika Kusini.

Faru hao wamepokelewa alfajiri Saa 9 jana katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kusafirishwa kwa ndege kuelekea Ikolongo-Grumet iliyopo Hifadhi ya Serengeti.

Aidha wakati Faru hao wakiwasili nchini, ilielezwa Faru mmoja alifariki akiwa Afrika Kusini wakati wa harakati za kuwasafirisha kuja nchini.

Hafla ya kuwapokea Faru hao ilihudhuriwa na viongozi mbalimabli wa Serikali wakiwamo Wakuu wa Mikoa ya Kilimanjaro Anna Mghwira na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za TANAPA, TFS, NCAA na TAWA, Wenyeviti wa Bodi wa mashirika hayo na viongozi wengine.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano kati ya serikali na Mfuko wa Grumet, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu alisema, serikali itahakikisha inawalinda wanyama hao kwa gharama yeyote.

“Faru hawa tutawalinda kwa gharama zozote iwe za kisanyansi au kienyeji,” alisema Naibu Waziri Kanyasu.

Kwa upande Kamishna Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Dk. James Wakibara alisema wanyama hao walikuwapo muda mrefu

Kutoweka kwao ni kwasababu ya matatizo ya ujangiri, baada ya juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Maliasili hatua inayofuatana sasa ni kuanza kuwarudisha,” alisema Dk. Wakibara.

Kamishna Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA Dk. Allan Kijazi alisema wamefarijika kupata Faru watakaoongeza idadi kwenye mfumo wa Ikolojia ya Serengeti.

Naye Kamishna Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi alisema kwa miaka mingi idadi ya Faru ilikuwa ikishuka Tanzania kwa hivyo mkakati uliowekwa mwaka huu ni kuongeza idadi ya Faru.

“Tunaamini mkakati wetu utafanikiwa kwa sababu nia ni kuongeza idadi ya Faru nchini,” alisema Dk. Manongi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...