Charles James, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT), Elirehema Kaaya amewataka vijana kuchangamkia fursa za kilimo badala ya kukaa vijiweni na kulalamika ajira hamna.

Kaaya amesema hayo wakati alipofika kukagua mradi wa kituo cha kilimo cha Kibakwe wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo alielezwa na wasimamizi wa kituo hiko juu ya uhaba wa vijana wanaoenda kujifunza kilimo.

Amesema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na halmashauri wamewekeza fedha nyingi ili kuboresha kituo hicho ili kiweze kutoa elimu kwa vijana na jamii inayozunguka eneo hilo.

" Vijana wengi wanapenda kazi za ofisini za kuvaa suti na tai lakini niwahakikishie kilimo kinalipa sana, mnapaswa mtumie fursa hizi ambazo Serikali inawaletea hadi maeneo yenu huku.

Alat tumeleta Sh.Milioni 150 na halmashauri imechangia karibu Sh.Milioni 90 ili kuandaa kitalu,mbogamboga na kutoa mafunzo kwa nguvu kazi ambapo wakulima wamepata elimu hiyo," Amesema Kaaya.

Kaaya ametoa maagizo kwa uongozi wa kituo hiko kujenga mfumo wa kuvuna maji ya mvua kwenye majengo ya kituo hiko ili kukabiliana na upungufu wa maji kwenye eneo hilo.

Nitoe wito kwa wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi kuhamasisha wanafunzi kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa elimu ambayo itakua msaada mkubwa kwenye maisha yao katika kuajiri.

Awali, akitoa taarifa ya kituo hicho, Mkuu kituo cha Kilimo, Taaluma na Mawasiliano Kibakwe, Samson German alisema kituo hicho kinatoa huduma za kilimo na mifugo kwa wakulima katika eneo husika.

“Wanaona kama kazi sio za kwao wanataka kazi zenye kipato kikubwa ambapo tunalazimika kupata vijana wa kufundishwa wanatoka mbali lakini wao wanaotoka hapa hawapatikani.Hata kazi za kupalilia ukimuita kijana wa eneo hili aje apalilie anaona kazi haimfai kwa sababu haina kipato kikubwa na kituo chetu hakina uwezo wa kuwalipa kiasi kikubwa," Amesema German.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT), Elirehema Kaaya akikagua shamba la mradi wa kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa.
 Katibu wa ALAT, Elirehema Kaaya akisikiliza maelezo juu ya mradi wa Kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa alipofika kukagua.
Katibu wa ALAT, Elirehema Kaaya akikagua shamba la Nyanya Chungu katika shamba la mradi wa Kilimo Kibakwe wilayani Mpwapwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...