Na Woinde Shizza Globu ya jamii,Arusha

Katika kuendeleza jitihada za kuunga mkono serikali katika ulinzi na
usalama hapa nchini Taasisi ya Fedha ya CRDB mkoani Arusha imetoa pikipiki tano kwa jeshi la Polisi wilayani Arumeru Mkoani Arusha lengo likiwa ni kuwarahisishia utendaji wa majukumu  kwa askari pindi wanapo hudumia wananchi.

Akiongea wakati akipokea pikipiki hizo pamoja na kuzindua rasmi zoezi la
ufanyaji wa doria ya kwanza ya ulinzi inayofanyika kwa  njia ya pikipiki
mkuu wa wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwapongeza wakurugenzi wa benki ya Crdb kwa kutoa pikipiki hizo kwani zitawasaidia  katika kufanya doria na ulinzi ili kuendelea kidumisha hali ya amani na usalama wa wananchi wao pia aliwapongeza kwa jinsi wanavyofanya kazi ya kuimarisha kazi ya utendaji kazi wa jeshi la polisi hapa nchini.

Alisema kuwa wilaya ya Arumeru ni wilaya nyenye kata nyingi na vijiji vingi
ambavyo vilikuwa vinaitaji huduma ya polisi hivyo pikipiki hizi
zitawasaidia kwa asilimia kubwa kufika katika vijiji hivyo na kutoa huduma
staiki kwa wananchi wote ,aidha pia alisema kuwA mbali na msaada huu wa
pikipiki tano wameshakarabati gari la polisi ambalo lilikuwa limekufa  ili
wananchi wote waweze kupata hiduma.

Alisema kuwa serikali haita lala itaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama
kwa raia unaendelea kwenda mbele ,pia alibainisha kuwa wataendelea
kuhakikisha ulinzi unaendelea kuimarka vyema ili mwananchi aweze kupata
maendeleo huku akibainisha maendeleo ya mwananchi hayawezi kuja bila kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha .

"mwananchi awezi kupata maendeleo akiwa na wasiwasi wa maisha yake
nanapenda kuwaambia na kuwahakikishia wananchi wangu usalama wa kutosha upo katika wilaya yenu ya Arumeru hivyo jengine majumba ,boresheni biashara zenu nunueni tv pamoja pia fanyeni jambo lolote linaloleta maendeleo  kwa amani kwani ulonzi wenu upo mikononi mwetu na ndio maana funasimama kwa ujasiri kabisa kwakusema hivi kuwa tutawalinda na tutaendelea kuwalinda mpaka hapo mungu atakapo amua mwenyewe nanawahakikishia amna mwananchi atakae kufa kwa bunduki ,wala kukabwa  na vibaka ,utakufa kwa kuchomwa
kisu  bali utakufa kwa mapenzi ya mungu"alisema Muro

Aidha Muro aliwataka askari polisi hao kutumia pikipiki hizo kwa malengo
yaliyopangwa katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao badala ya kuzitumia kwa maslahi yao binafsi .

"nyie askari msitumie pikipiki hizi kwa ajili ya kujitafutia kipato ambacho
sio halali ,au kufanya pikipiki hizi kama nizakwenu fanyeni kazi
zilizokusudiwa kufanywa na pikipiki hizi"alisema Muro

Akikabidhi pikipiki hizi  mkurugenzi wa wawateja wadogo mkoa wa Arusha Boma Rabala alisema kuwa ni jambo la wazi kuwa umakini wa jeshi la polisi ni chachu kubwa ya maendeleo ya taifa letu na juhudi za jeshi hili zimechangia katika kutengeneza mazingira rafiki na salama miongoni mwa jamii na hivyo kuwa kichocheo cha kukua kwa shughuli za uzalishaji mali .

Alisema kuwa benki inatambua na kuthamini sana wa usalama wa raia namali zao ,pia wanatambua kuwa taifa bora ni taifa lenye usalama wa raia na mali zao ,na sio usalama tu bali usalama wenye uhakika ambao uwapa wananchi amani ya uzalishaji huku wakijua familia zao zipo salama kinyume cha hapo juhudi za kujikwamua kutoka katika umaskini hazitafanikiwa.

"benki yetu inatambua kuwa ili jeshi la polisi liweze kufanya kazi zake kwa
ufanisi zaidi ,linahitaji vifaa na miundombinu iliobora na kutokana na hilo
sisi tukiwa kama sehemu ya jamii na mdau mkubwa wa maendeleo tumekuwa tukiboresha katika kuboresha utendaji wa jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali ya jamii na ndio maana leo tumeona tutoe pikipiki hizi kwa kwa kituo cha polisi cha usa river ambacho kitaudumia wilaya ya Arumeru nzima"alisema Rabala

Nae meneja wa kanda wa benki ya CRDB Chiku Issa alisema kuwa wametoa
pikipiki tano aina ya TVS zenye thamani ya  shilingi milioni 10  ambapo
alibainisha kuwa anatumaini pikipiki hizi zitaweza kusaidia kutatuawa
changamoto ya usafiri ilikuwepo na hivyo kuongeza ufanisi kwa askari katika kupambana na uhalifu.
 pikipiki zilizotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya doria zikiwa zimepaki nje ya kituo cha polisi  Usariver kabla ya makabidhiano
 wafanyakazi wa benki ya CRDB wakifuaitlia kwa makini zoezi la akabidhiano ya pikipiki lililofanyika nje ya kituo cha polisi Usariver  
 mkuu wa wilaya ya Arumeru akikata utepe ishara ya kupokea pikipiki zilizotolewa na CRDB pamoja na ishara ya uzinduzi rasmi wa doria ya pikipiki wilayani humo
 Kaimu mMrakibu wa polisi wilaya ya Arumeru  David Mapunda  akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo na mkuu wa wilaya ambapo aliahidi kwa kusema pikipiki hizo zitatumika kwa kazi iliyokusudiwa .

wakwanza kushoto ni kaimu mrakimu wa polisi wilaya ya Arumeru  David Mapunda wa pili kushoto mkuu wa wilaya ya Arumru Jerry muro  ,wakwanza kulia ni Mrakibu msaidizi mwandamizi wa polisi kituo cha Usariver Fatuma Wiliam wapili kulia  ni mkurugenzi wa wawateja wadogo mkoa wa Arusha Boma Rabala wote wakiwasha pikipiki ishara ya kuzindua rasmi doria ya kwanza ya pikipiki kwa askari wa wilaya ya Arumeru .

 mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye pia ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya yake  akiwa anajaribu (test) moja ya pikipiki zilizotolewa na  benki ya CRDB kwa ajili ya kufanyia doria katika wilaya ya Arumeru. 
 kikosi cha polisi cha doria  kikiondoka katika eneo la kituo cha polisi Usariver mara baada ya kupatiwa pikipiki tayari kabisa kwa ajili ya kuanza doria  ya kulinda wananchi wake .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...