Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

LEO OKtoba 23, Waziri wa Ulinzi na Jesh la kujenga Taifa Dkt. Hussein Ally Mwinyi amezindua rasmi idara na jengo la kusafisha figo katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo Waziri Mwinyi amesema ukamilikaji wa kituo hicho umefika muda sahihi kwa kuwa unaenda sambamba na mlengo wa Serikali wa kujenga vituo vya afya kote nchini.

"Serikali ya awamu ya tano imeendelelea kuhakikisha vituo vya afya vinajengwa kote nchini na kukamilika kwa kituo hiki utarahisisha utoaji huduma kwa wananchi pia utapunguza gharama kwa kuwapeleka wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwani tunaamini tutawapokea wagonjwa wengi " ameeleza.

Amesema kuwa huduma zinazotolewa na Jeshi ikiwemo elimu na afya si kwa jeshi na familia zao bali ni kwa jamii nzima hivyo watumie fursa hizo kwani ni kwa ajili ya wote.

Pia amewataka wataalamu watakaoendesha huduma hiyo kutumia vifaa hivyo kwa uangalifu ili kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi na kuvifanya vifaa hivyo vidumu kwa muda mrefu zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama nchini Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jeshi na jamii kwa ujumla.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2016 na kumalizika 2017 na  Rais Dkt. John Joseph Magufuli alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na hadi kukamilika kwake kimegharimu shilingi Milioni 431, laki nane ishirini na saba elfu mia tisa na thelathini na tano na tayari lina mashine bora zilizonunuliwa nchini ujerumani kwa gharama ya shilingi milioni 633 huku wakiwa na mpango wa kujenga kituo cha utambuzi kwa wagonjwa (diagnosis centre.)

Amesema kuwa kituo hicho ni cha kwanza kuwepo jeshini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964 na hiyo itasaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya taifa Muhimbili pamoja ma kuipunguzia gharama serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho Daktari bingwa wa magonjwa ya pua, koo na masikio na msimamizi Mkuu wa hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Brigedia Jenerali Gabriel Mhidze amesema kuna wataalamu wa kutosha pamoja na mashine kumi za kuchuja wagonjwa wa figo na hadi sasa wamefanya michujo kumi na tisa huku wakiwa na uwezo wa kuwahudumia wagonjwa arobaini kwa siku.

Amesema kuwa gharama kwa huduma hiyo ni nafuu na amewashauri wananchi kufuata sheria za afya ili kuepukana na tatizo la figo ikiwemo kuzingatia vyakula pamoja na kucheki afya zao ili kujilinda zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...